Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini |
Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir, amelivunja
baraza lake la mawaziri pamoja na kumfuta kazi makamu wa rais Riak Machar
katika mabadiliko makubwa zaidi kuwahi kutekelezwa katika historia ya miaka
miwili ya taifa hilo.
Aliyekuwa
waziri wa habari, Barnaba Marial Benjamin, ameiambia BBC kuwa mawaziri wote
kutoka kwa Makamu wa Rais Riek Machar wameondolewa.
Duru
zinasema haijabainika iwapo kuna waziri yeyote miongoni mwa wale waliofutwa
kazi atarejeshwa katika baraza jipya la mawaziri litakalobuniwa.
Pia
hakuna sababu iliyotolewa kuhusiana na hatua ya rais kuwafuta kazi maafisa hao ,
lakini wadadisi wanasema kuwa Bwana Kiir na makamu wake Machar wamekuwa na
mgogoro wa mamlaka kwa miezi kadhaa sasa.
Sudan
Kusini imekumbwa na matatizo chungu nzima hasa ya kiuchumi tangu kujitenga na
Sudan mwaka 2011.
Uthabiti
wake umetatizwa na malumbano kati yake na Sudan kuhusu mipaka na swala la
mafuta.
Hivi
karibuni baadhi ya maafisa wa Bwana Kiir, wamekuwa wakizungumzia kuwepo
minong'ono kuhusu uongozi wake.
Ripoti
zinasema kuwa Kiir anajitahidi kusalia na ushawishi katikachama cha Sudan
People's Liberation Movement (SPLM), ambacho kinathibiti serikali.
Kwa
upande wake bwana Machar, ambaye mwezi Aprili alipunguziwa mamlaka, alisema
huenda akagombea uongozi wa chama cha SPLM dhidi ya rais Kiir, kabla ya uchaguzi
mkuu utakaofanyika mwaka 2015.
No comments:
Post a Comment