Shirika
la Msalaba Mwekundu nchini Tanzania (TRCS) litasambaza vyandarua 68,000
vilivyowekwa dawa ya kuua mbu kwa wakimbizi wanaoishi kwenye kambi ya Nyarugusu
mkoani Kigoma.
Shirikisho
la Kimataifa la Msalaba Mwekundu na Mwezi Mwekundu linafadhili usambazaji huo,
ambao utaanza tarehe 30 Julai kwa kushirikiana na kampeni ya Wakfu wa Umoja wa
Mataifa ya "Si Chochote ila Vyandarua tu" na mashirika washirika ya
misaada.
"Malaria
ni ugonjwa pekee inaouwa watu wengi kabisa kwenye kambi hii ya wakimbizi,
yakiwaathiri zaidi wanawake wajawazito na watoto walio chini ya umri wa miaka
mitano," alisema Rais wa TRCS, George Nangale.
Zaidi
ya matukio 11,000 yalirikodiwa kwenye kambi hiyo kati ya mwezi Januari na
Aprili mwaka huu, na malaria ni sababu ya asilimia 60 ya matibabu ya kiafya,
alisema.
Wengi
wa wakimbizi kwenye kambi ya Nyarugusu wanatoka Burundi na Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo.
No comments:
Post a Comment