Mhadhiri
Mwandamizi wa Chuo cha Uhasibu Arusha na Mchumi, Balozi Morwa alitoa
mapendekezo hayo juzi, wakati akiwasilisha utafiti kuhusu wajibu wa kampuni kwa
jamii(CSR),uliofanyika katika machimbo ya Tanzanite Mirerani, wilayani
Simanjiro Mkoa wa Manyara.
ARUSHA, Tanzania:
Serikali
imeshauriwa kubadili sera ya uwekezaji nchini kwa kulazimisha kisheria kampuni
za wawekezaji hasa wa Sekta ya Madini, kutekeleza miradi ya jamii inayozunguka
maeneo yao ya uchimbaji badala ya suala hilo kuwa ni la hiari.
Mhadhiri
Mwandamizi wa Chuo cha Uhasibu Arusha na Mchumi, Balozi Morwa alitoa mapendekezo
hayo juzi, wakati akiwasilisha utafiti kuhusu wajibu wa kampuni kwa
jamii(CSR),uliofanyika katika machimbo ya Tanzanite Mirerani, wilayani
Simanjiro Mkoa wa Manyara.
Morwa
akiwasilisha utafiti huo ,ambao uliratibiwa na Mtandao wa Mashirika yasiyo ya
kiserikali ya Mkoa wa Arusha kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la
Finnish NGO Platform, alisema wamebaini kuwa jamii zinazozunguka migodi ya
Tanzanite hazinufaiki ipasavyo.
Morwa
alisema utafiti huo, ulihoji watu 350 na nyaraka kukusanywa,wamebaini,wajibu wa
kampuni ya wawekezaji kwa jamii ukiwa wa kisheria kama Ghana, utawanufaisha na
ikishindika ifutwe na kampuni hizo zilipe kodi kubwa kama nchi nyingine.
No comments:
Post a Comment