KUHUSU KAMANDA LWAKATARE; PRESS CONFERENSE NA MIKUTANO YA KAMPENI
Kumekuwepo na taarifa zinazosambazwa kwa njia
mbalimbali za upashanaji habari tangu jana juu ya vitu viwili ambavyo vyote
vinamhusu Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA, Ndugu Wilfred Mganyizi
Lwakatare.
1. Kwamba atafanya press conference leo, (watu wale wa
upande wa pili wameenda mbali hata wametaja muda eti ni saa 4 asubuhi)
2. Atakuwa kwenye mizunguko ya mikutano ya kampeni
katika chaguzi ndogo za udiwani zinazoendelea katika hatua ya lala salama
maeneo mbalimbali nchini.
Usahihi.
Kwa kuzingatia masuala kadhaa hasa mikakati ya
kitaalam katika mapambano ya kisiasa, hususan katika suala hili, press
conferense iliahirishwa tangu jana mapema asubuhi, baada tu ya baadhi ya vyombo
vya habari kuwa vimetangaza kuwa itafanyika leo, Alhamis. Tuliviarifu vyombo
vya habari hivyo. Imesogezwa mbele na taarifa zitatolewa tena.
Suala la mizunguko kwenye kampeni za uchaguzi
mdogo...hakuna kitu kama hicho kwa sasa.
Pamoja na kwamba kuna watu wenye mapenzi mema
kabisa na vuguvugu la mabadiliko wamekuwa na hamu ya kutaka kumsikia kamanda
mwenzao, ndugu Lwakatare akizungumza majukwaani baada ya miezi mitatu ya
'ukatili' mkubwa, pia tumebaini kuwa watu wa upande wa pili, wanataka sana
kujua CHADEMA sasa inajua kiasi gani juu ya njama za kuibambikia ugaidi,
utekaji na mauaji.
Hivyo upande huo wa pili, ambao unaonekana dhahiri
kuwa under pressure ya kutojua kiasi gani mipango yao inajulikana na
itaumbuliwa kwa kiwango kipi, umekuwa ukieneza habari za Lwakatare kufanya
mikutano ya hadhara kwenye kampeni za uchaguzi wa madiwani, kitu ambacho si
kweli.
Baada ya hila na uovu wa watawala na vibaraka wao
kushindwa katika jaribio lingine kubwa kabisa wao kuwahi kupanga dhidi ya wimbi
la mabadiliko na kutaka kuzuia kasi ya CHADEMA kuwaondoa madarakani, tumwache
ndugu Lwakatare apumzike na familia, wakati mipango makini ikifanywa kwa ajili
ya matukio yote mawili ambayo Watanzania wanategemea na kuyasubiri kwa hamu
yafanyike; mkutano na press conference.
Kitu kimoja cha uhakika ni kwamba, watu wa upande
wa pili, ambao tayari hofu yao inajulikana, hawataweza kumchagulia Lwakatare
wala kuichagulia CHADEMA kitu gani cha kusema, kama ambavyo wameanza kufanya
kupitia forums mbalimbali. Let tthem cool down, wasiwasi wa nini! Yote
yakayosemwa itakuwa ni kwa ajili ya maslahi ya Watanzania, haitakuwa kwa ajili
ya kuifurahisha 'status quo'.
Ukweli haujawahi kushindwa na uongo, wala dhuluma
haijawahi kuishinda haki. Vyote viwili, ukweli na haki, vinaweza kuchelewa tu,
lakini hatimaye huwadia. Kwa sababu Lila na Fila havitangamani.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari - CHADEMA
Alhamis, Juni 13, 2013.
No comments:
Post a Comment