Mlipuko wa hivi karibuni wa malaria mkoani Kagera, Tanzania, ulikuwa tu kwenye vijiji ambavyo havikujumuishwa kwenye Programu ya Kupuliza Dawa Majumbani, liliripoti gazeti la Daily News la Tanzania siku ya Jumatatu (tarehe 10 Juni).
Serikali
imetuma timu ya watalaamu kwenye eneo hilo kuchunguza mlipuko huo wa malaria,
ambao umeshaua kiasi cha watu 20, wengi wao watoto wadogo, tangu mwishoni mwa
mwezi Mei. Vile vile, Wizara ya Afya, imeagiza dawa zaidi kutumwa kwenye
hospitali ya karibu ya Rubya, ikikanusha taarifa kwamba mlipuko huo ulisababishwa
na upungufu wa vidonge vya kupambana na malaria.
Kila
siku kiasi cha watu 30 hadi 40 hufika Hospitali ya Rubya wakiwa na malaria.
Wastani wa mtoto mmoja hadi wawili hufa kila siku, alisema Afisa wa Matibabu
Hospitali ya Rubya, Diocles Ngaiza. "Katika siku ya kwanza ya mlipuko,
vilirikodiwa vifo 16, vingi vikiwa vimesababishwa na watoto hao kufikishwa
hospitalini ikiwa wameshachelewa sana," alisema.
No comments:
Post a Comment