Polis nchini Ghana wamewatia nguvuni watu 55
raia wa nchi mbali mbali kutoka Afrika Magharibi wanaoshukiwa kuendesha
shughuli haramu za uchimbaji haramu wa dhahabu, msemaji wa wizara ya uhamiaji
alisema.
Kukamatwa
kwao kunaashiria kuwa polisi wameelekeza nguvu zao sasa kwa wahamiaji wa
Kiafrika kutoka kwa Wachina kama anavyo ripoti mwandishi wa BBC Akwesi Sapong
akiwa nchini Ghana.
Serikali
hiyo ya Ghana iliwaachilia washukiwa 124 raia wa Uchina wikendi na kuwaamuru
waondoke nchini humo mara moja. Sheria
za Ghana zimeharamisha mwananchi yeyote wa kigeni kuajiriwa katika migodi
midogo midogo ya nchi hiyo. Ghana
ndio nchi ya pili kwa uzalishaji mkubwa wa dhahabu barani Afrika baada ya
Afrika Kusini.
MWINGILIO WA UCHINA
Wachina
watoa dhahabu Ghana
|
Kukamatwa
kwa wageni imepokewa vizuri na raia wa Ghana masikini wanaoamini kuwa
wafanyikazi kutoka nje wanadakia nafasi zao za ajira, kwa mujibu wa mwandishi
wetu.
Msemaji
wa wizara ya Uhamiaji Francis Palmdeti ameambia BBC kuwa kati ya 55 waliokamatwa,
51 ni raia wa Niger, 3 wametoka Togo na mmoja kutoka Nigeria.
Wachina waliokamatwa Ghana |
'Bado
uchunguzi unafanywa wa asili ya washukiwa wengine watatu baada wamedai kuwa
raia wa Ghana na kukana kuwa wametoka Mali kama tulivyo shuku awali' amesema
msemaji huyo.
Mwandishi
wa BBC anasema kuwa oparesheni kama hii inamaanisha kuwa serikali imeazimia
kumaliza uajiri wa mtu yeyote ambaye siye raia wa Ghana katika machimbo ya nchi
hiyo.
No comments:
Post a Comment