Maofisa wa usalama wa Kenya Jumatatu wakionyesha
silaha zilizokamatwa wakati wa mapigano ya koo katika wilaya ya Rhamu, Kaunti
ya Mandera.
|
Polisi
huko kaskazini mashariki mwa Kenya wameimarisha usalama katika kaunti ya Wajir
kuzuia vurugu zilizoenea kutoka Kaunti jirani ya Mandera baina ya koo za
Degodia na Gare.
Vurugu
za hivi karibuni ziliibuka huko Wajir zilianza Ijumaa iliyopita (tarehe 21
Juni) wakati wanaume washukiwa wa koo za Degodia walipovamia malori mawili
katika kijiji cha Eldas, na kuua wanaume wanne wa koo za Gare, Mkuu wa Kaunti
ya Wajir Naftali Mung'athia alisema.
Katika
kulipiza kisasi kwa mfululizo wa mashambulio ya hivi karibuni dhidi ya Gare, wanaume
wenye silaha walivamia kambi ya watu wasio na makazi ndani ya nchi katika
wilaya ya Banisa ya Kaunti ya Mandera, na kuua watu 14 ikiwa ni pamoja na ofisa
polisi Jumapili. Waliokufa, ni pamoja na wanawake na watoto, wote kutoka ukoo
wa Degodia.
Baadhi ya Familia zilizokosa makazi. |
Jumatatu,
kundi la watu kutoka katika ukoo wa Degodia waliwalenga watu kutoka ukoo wa
Gare katika ghasia kwenye mji wa Wajir, walimuua mwanamke mmoja na mwingine
kujeruhiwa vibaya baada ya kukanyagwa na msafara uiokuwa ukibeba familia
zilizokuwa zikikimbia vurugu hizo.
Kuepusha
mapigano zaidi baina ya koo mbili hizo, mamlaka zinazohusika zimesambaza
maofisa usalama na askari katika viunga vyote vya jirani na Wajir, Mung'athia
alisema. Alitoa wito kwa wakaazi wa Wajir kuwa watulivu wakati serikali ya
Kaunti ikifanya kazi kutatua mzozo huu, akiongezea kwamba upigaji marufuku wa
muda wa mikusanyiko imetekelezwa.
"Tunafanya
kazi mchana na usiku kuzuia mzozo kutokuendelea," Mung'athia alisema.
"Tumewataka viongozi wa ndani na maulamaa kuungana katika kurejesha amani
baina ya koo hizi."
Historia yenye vurugu
Wimbi
la hivi karibuni la vurugu hizi lilianza mwezi Machi wakati wa gari la kampeni
linalomilikiwa na mgombea seneta Billow Kerrow, ambaye anatoka katika ukoo wa
Gare, lilipomgonga na kumuua mfanyabiashara kutoka katika ukoo wa Degodia huko
Rhamu. Baadhi ya wanachama wa jumuiya ya Degodia walidai ajali ilikuwa
imepangwa.
Kutoka
hapo, mapigano ya koo, na mashambulizi ya kulipiza kisasi yameshaua watu zaidi
ya 50 na kufanya mamia ya familia kukosa makazi.
Vurugu
baina ya koo mbili hizio yamekuwa yakipamba moto siku hadi siku, na yalianza
kuongezeka kutoka mwaka 1984 wakati ukame uliposababisha mzozo wa maeneo ya
malisho, kwa mujibu wa Mkuu wa Kaunti ya Mandera Michael ole Tialal.
Gare
ni ukoo unaotawala huko Mandera, wakati Degodia ni wengi huko Wajir.
Usambazaji
mdogo wa maji na ardhi ya malisho yamekuwa ni maeneo ya mzozano kati ya koo
hizo, Tialal alisema, akiongeza kwamba kuenea kwa bunduki katika mpaka wa
Somalia na Ethiopia kumeongeza vurugu katika tatizo la usalama la mkoa.
"Ni
mara ya kwanza kwa ukoo kutumia chombo cha kurushia maguruneti katika mapigano
yao ya koo," Tialal alisema, akirejea shambulio kwenye kambi katika wilaya
ya Banisa. "Vurugu hizo pia zilihusisha kuchoma nyumba na kuvamia
magari."
"Kwa
sasa tunatoa kikundi cha walinzi cha wasindikizaji wenye silaha na magari
yanashauriwa kusafiri kwa kusindikizwa na ulinzi ili kupunguza [uwezekano wa]
shambulio,".
Siku
ya Jumatatu, Inspekta Jenerali wa Polisi wa Kenya David Kimaiyo aliwaita
viongozi waliochaguliwa wa kaunti za Mandera na Wajir katika idara ya Uchunguzi
wa Makosa ya Jinai kuhusiana na ripoti za upelelezi zikionyesha kwamba
mashambulizi "yalichochewa kisiasa".
Baada
ya kukutana Nairobi siku ya Jumatatu na viongozi wa kaunti zote mbili, Rais
Uhuru Kenyatta alisema serikali ya Kenya inaweza kutumia nguvu kurejesha amani
katika mkoa wa kaskazini-mashariki, akiagiza jamii zinazopigana kusalimisha
silaha haramu.
"Kama
jamii za kaunti za Mandera na Wajir hawatarejesha amani wao wenyewe, serikali
itakuwa haina lingine la kufanya bali kutumia operesheni ya ulinzi ambayo
inaweza kutokuwa na matokeo yasiyodhamiriwa," rais alisema.
Pia
Kenyatta aliahidi kufanya kazi na serikali ya Ethiopia kuhakikisha kuishi
pamoja kwa amani miongoni mwa jamii nyingine za kikabila zilizoenea katika mkoa
ambako mipaka ya Kenya, Ethiopia na Somalia inakutana.
Rasilimali, siasa za mafuta zaleta ugomvi
Licha
ya jitihada za kuzuia vurugu katika ngazi za kaunti na taifa, mlipuko wa vurugu
umeendelea kujitokeza.
Siku
ya Jumanne (tarehe 25 Juni), viongozi wa ulinzi katika kijiji cha Guba
walimpiga mtu mmoja risasi na kumuua wakati wakipigana na wanaukoo wenye silaha
ambao walikuwa wanatuhumiwa kupanga shambulizi kwa wanakijiji, alisema Naibu wa
Mkuu wa Kaunti ya Mandera Sammy Mwati.
Katika
miezi iliyopita, vikosi vya usalama viliwakamata watu zaidi ya 90 kuhusiana na
mashambulizi hayo, Mwati alisema, na baadhi ya viongozi wa jamii pia wamekuwa
wakihojiwa kwa kutuhumiwa kuhusika katika mapigano.
Sheikh
Mohamed Deeq, imamu wa msikiti wa Jamia Salaam katika mji wa Wajir, alisema
baadhi ya viongozi wa jamii wanachochea mgogoro kupitia kauli za kuchochea.
"Baadhi
ya viongozi wa jamii kutoka katika mkoa huo sio wakweli kwa wito wao wa
amani," aliiambia Sabahi. Viongozi wanahubiri amani lakini wanachochea
vita kwa kujificha na katika mioyo yao."
Ingawa
viongozi wa dini wamekutana kusaidia kurejesha utulivu katika kaunti zote,
jitihada kubwa inahitajika, alisema.
"Kama
viongozi wa dini, inaonyesha pia hatukutimiza wajibu wetu kikamilifu,"
alisema. "Tutakutana kama viongozi wa dini mara moja kutathmini mafundisho
yetu. Tunahitaji sana kuboresha jitihada zetu katika kuwafundisha watu
mafundisho ya Mungu."
Utatuzi wa Kimila kwa vurugu za koo
Magavana
wa kaunti hizo mbili pia wanashirikiana kumaliza vurugu.
Gavana
wa Kaunti ya Wajir Ahmed Abdullahi na Gavana wa Kaunti ya Mandera Ali Ibrahim
Roba walikubaliana wakati walipokutana na Kimaiyo tarehe 28 Mei kuwazuia watu
wa koo zao kufanya vurugu. Wametoa wito pia kukomeshwa mara moja vurugu za kikabila katika Kaunti
ya Mandera.
"Kuna
faini ya shilingi milioni 10 (dola 116,000) kwa jamii nzima itakayochochea
vurugu," Abdullahi aliiambia Sabahi. "Serikali ilipaswa kutekeleza
mapendekezo na tunaunga mkono."
Faini
inazingatiwa kamamaslah, kitendo cha kimila kinachofanyika huko kaskazini
mashariki nchini Kenya ambako familia zilizopoteza wapendwa wao katika vurugu
za kikabila zinapata malipo kwa ajili ya uharibifu kutoka katika ukoo unaokwaza,
alisema.
"Mgogoro
huu unatutishia kutofanya shughuli za maendeleo kwa ufanisi," Roba
aliiambia Sabahi. "Ndiyo sababu mimi binafsi ninajitolea kumaliza
vurugu."
Aidha,
jamii zote zitazingatiwa katika kazi za serikali za kaunti na kuingizwa katika
ajenda ya maendeleo, alisema.
Familia
za Degodia ambazo zilikimbia makazi yoa kwa sababu ya vurugu za koo zimekuwa
zikikaaa katika kambi nje ya ofisi za mkuu wa wilaya ya Rhamu katika Kaunti ya
Mandera tangu mwezi Machi.
Ibrahim
Kullow Ahmed, mkaazi wa Rhamu mwenye umri wa miaka 24, alisema alikimbia makazi
yake kwa sababu yeye na majirani zake walikuwa wakiishi wakiwa na hofu ya
kushambuliwa.
"Nyumba
zetu zilichomwa moto na sasa tumepiga kambi katika ofisi za serikali za
mitaa," aliiambia Sabahi. "Watu wanahofu sana kwa sababu mashambulizi
yanafanyika hata mchana."
"Watoto
wanakabiliana na wasiwasi usiku na misikitini," alisema, akiongeza kwamba
wanakosa chakula na maji.
Info Source: Sabahi Online
No comments:
Post a Comment