To Chat with me click here

Thursday, June 27, 2013

UCHAGUZI MKOANI ARUSHA WAAHIRISHWA BAADA YA MLIPUKO WA BOMU



Mwk. wa NEC, Damian Lubuva

Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania (NEC) imeusogeza mbele uchaguzi kwenye wadi nne za Arusha kutoka tarehe 30 Juni hadi 14 Julai ili hali itulie, liliripoti gazeti la Daily News la Tanzania siku ya Jumatano (tarehe 26 Juni).

Uchaguzi huo uliahirishwa kutokana na ghasia zinazoendelea baada ya mlipuko wa bomu kwenye mkutano wa kampeni wa chama cha upinzani cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mapema mwezi huu.

"Kwa bahati mbaya tumegundua kwamba hali bado haijakuwa sawa na inahitaji muda zaidi kuchunguzwa," alisema Mwenyekiti wa NEC, Damian Lubuva. "Tunataka watu wapige kura kwa amani ... Wapiga kura wanaweza kufanya maamuzi yasiyo busara au yatokanayo na taarifa mbaya ikiwa watapiga kura katika hali ya wasiwasi."

Lubuva aliwakumbusha wagombea na vyama kwamba uahirishaji huo haukukusudiwa kuruhusu kampeni zaidi kuendelea.

No comments:

Post a Comment