Mandela
na Winnie, katika siku za furaha
|
Mke wa zamani wa Nelson Mandela, Winnie
amewasili katika hospitali nchini Afrika Kusini, ambako inaaminiwa rais huyo
mstaafu anaendelea kupokea matibabu kwa ugonjwa wa homa ya mapafu.
Mtoto wao wa kike Zenani (mandela -
Dlamini) pia amerejea nchini Afrika Kusini kutoka Argentina ambako anahudumu
kama balozi wa Afrika Kusini, ili awe na babake.
Bwana Mandela, mwenye umri wa miaka 94,
alipelekwa hospitalini mapema Jumamosi , ikiwa ni mara ya tatu kulazwa
hospitalini mwaka huu.
Kwa mujibu wa duru za urais, Mandela
amekuwa akiugua kwa muda mjini Johannesburg baada ya kukumbwa tena na ugonjwa
wa mapafu. Msemaji wa serikali Mac Maharaj amesema kuwa maafisa katika
hospitali wanataka kudhibiti idadi ya watu wanaozuru hospitali hiyo ili
wampunguzie bwana Mandela usumbufu.
Risala za heri |
Alilazwa hospitalini baada ya hali yake
kuwa mbaya zaidi mnamo Jumamosi. Kwa mujibu wa taarifa za urais, Rais
President Jacob Zuma, amerejelea wito wake kwa watu nchini Afrika Kusini
kumuombea Madiba wakati huu anapougua.
Lakini mwandishi wa BBC mjini Pretoria,
Karen Allen, anasema kuwa kuna matumaini madogo kuwa Mandela aliyeongoza vita
dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi, huenda akapona.
Anasema kuwa wengi walipata matumani
baada ya bintiye Mandela Zindzi, kusema kuwa babake yuko salama na kuwa
anaendelea kupata nafuu. Mkewe Mandela Graca Machel, alifutilia
mbali, ziara yake mjini London Jumamosi ili kuwa kando ya mumewe.
Mandela alikuwa Rais wa Afrika Kusini
kati ya mwaka 1994 hadi 1999. Alifungwa jela miaka 27 na anaaminika
kuwahi kuugua ugonjwa wa mapafu alipokuwa akifanyishwa kazi ngumu katika
machimbo ya mawe akiwa jela.
No comments:
Post a Comment