MIGIRO MAKAMU MWENYEKITI,
NAPE KATIBU MKUU,
NGELEJA KATIBU MWENEZI.
UONGOZI mpya wa CCM sasa
uko ndani ya bahasha. Kilichobaki ni uamuzi wa kura za wajumbe wa Halmashauri
Kuu ya Taifa ( NEC ) kufungua bahasha hiyo na kuweka siri hiyo wazi.
Kumalizika kwa vikao vikuu vya chama kunatoa taswira ya uongozi mpya wa CCM, hasa kuzingatia kilio cha muda mrefu kutoka kwa wanachama kuisihi CCM irejee kwenye uasilia wake.
Sasa ni sura mpya na taswira mpya. Kauli ya Mwenyekiti Taifa, Rais Kikwete kuwa “Hatuwezi kuwa na Chama cha wazee tu, hapana, tumeona tuwape nafasi vijana wengi, tena wasomi waweze kugombea…Ni muhimu kupata sura mpya ya chama na taswira mpya kwa kuingiza wasomi”, ni kauli inayoashiria mabadiliko makubwa katika CCM yanayotarajiwa.
Anaendelea kusisitiza akiwaeleza wajumbe wa NEC, kuwa “lengo ni kuunda timu ya ushindi ya Chama kwa mwaka 2014 katika uchaguzi wa Serikali za mitaa, na mwaka 2015 katika Uchaguzi Mkuu.”
Nasaha kwa wale “wenye ndimimbili” anasema kuwa “isiwe nongwa ukiwa basi ni kulalamikia chama hiki kimefanya nini, ukishafikia hivyo wewe haukuwa na moyo na chama ila moyo wako ulikuwa na shida ya uongozi.”
Wakati hali ikijiri hivyo, hali ndani ya chama inaripotiwa kuwa ni tulivu hata mara baada ya kupita panga la kung’oa visiki, hii ikiashiria kuwa sasa chama kinajivua ‘gamba’, na hii imepokewa kwa shangwe na furaha na wana-CCM wengi.