To Chat with me click here

Friday, May 3, 2013

MBOWE: MAJANGILI SASA WANASAGA MENO YA TEMBO


Mhe. Freeman Mbowe, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni.

Mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii ilizidi kulitikisa Bunge baada ya jana Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe kusema kwamba kuna kwa viwanda vinavyosaga meno ya tembo kabla ya kuyasafirisha nje.

Akichangia hotuba ya wizara hiyo, Mbowe alisema majangili wamekuja na mbinu hiyo mpya kwa lengo la kukwepa kunaswa na vyombo vya dola. Alisema hivi sasa meno hayo hayasafirishwi kwa meli kama zamani na badala yake kuna viwanda nchini ambavyo huyasaga meno hayo na kisha kusafirishwa kama unga kupitia viwanja vya ndege.

“Watu hawa wamekuwa wajanja, wameona kupitisha meno kama unga ni rahisi kwani hakuna mashine za kung’amua unga huo,” alisema Mbowe.

Mbowe alisema Serikali inapaswa kuwa na mikakati ya kukabiliana na biashara hiyo ambayo inaweza kuwamaliza tembo wa Tanzania. Mbowe alisema kwa sasa kilo moja ya meno ya ndovu inauzwa mpaka Dola 5,000 (Sh7.9 milioni), jambo linalofanya majangili kubuni njia mbalimbali za kufanikisha njama zao.

Alishauri kuwa Serikali inapaswa kuchukua hatua kali dhidi majangili ikiwamo ya kuwanyonga wanapopatikana na hatia.

“Tatizo wahusika wakubwa wa biashara hii ni watu wenye uhusiano mkubwa na viongozi wa Serikali lakini dawa yao ni kunyonga tu,” alisema.

Kauli hiyo ya Mbowe imekuja siku chache baada ya Msemaji wa Kambi ya Upinzani katika Wizara ya Maliasili, ambaye pia ni Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Peter Msigwa kutoa tuhuma nzito kwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwamba anahusika na biashara ya meno hayo.

Jana, akichangia mjadala wa bajeti hiyo, Msigwa alimjia juu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi kwa kitendo chake cha kumtetea Kinana badala ya kumtaka kumpa ushahidi wa tuhuma alizotoa.

“Nilitarajia Nchimbi angenitaka nimpelekee ushahidi badala yake, anamkingia kifua mtuhumiwa, lakini sishangazwi na maelezo yake kwa sababu aliweza kuitwa Dokta kabla hajapata shahada,” alisema.
 
Alisema badala ya wapinzani kuitwa wahuni, wabunge wa CCM walitakiwa kufanya kazi pamoja kuhakikisha wanalinda masilahi ya nchi.

Hata hivyo, akichangia hoja hiyo, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole Medeye alimtetea Kinana na kuiomba Ofisi ya Bunge kuielekeza wizara inayohusika na usafirishaji kutoa semina kwa wabunge wa upinzani akisema wengi hawajui taratibu za kusafirisha mizigo.

“Sikufurahishwa kabisa na kauli ya Mchungaji Msigwa kwa kuwataja viongozi kuhusika na biashara ya meno ya tembo licha ya ukweli kuwa kuna mfumo wa mambo ya usafirishaji,” alisema Medeye.

Thursday, May 2, 2013

TUHUMA: VIGOGO, WAKALIA MABILIONI YA CIS



Mhe. Kimbisa
Dar es Salaam. Baadhi ya wanasiasa, wafanyabiashara na wizara kadhaa za Serikali za Muungano na ile ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), wameendelea kukalia mabilioni ya shilingi waliyokopa kupitia uliokuwa Mfuko wa Kuwezesha Uagizaji Bidhaa kutoka nje ya Nchi (Commodity Import Support - CIS).

Taarifa ambazo zimetufikia zinasema kiasi cha fedha ambacho bado hakijarejeshwa na wakopaji hao ni Sh216 bilioni ambazo kama zingepatikana, zingetosha kugharimia madawati milioni 2.7 kwa gharama ya Sh80,000 kila moja yenye uwezo wa kutosheleza wanafunzi milioni 8.1.

CIS ni mpango ulioanzishwa na Serikali miaka ya 1980 na kuendelea hadi mwanzoni mwa miaka 2000, ambao nchi wahisani zikiongozwa na Japan zilikuwa zikiipatia Serikali fedha za kigeni ili kuimarisha sekta za biashara.

Nchi nyingine zilizochangia fedha hizo ni Uingereza, Uholanzi, Saudi Arabia, Norway, Uswisi, Ubelgiji, Sweden na Denmark na madeni yaliyotokana na fedha hizo ni sehemu ya deni la taifa ambalo linagharimiwa na fedha za walipakodi wa sasa.

Hata hivyo, taarifa zilizopo zinaonyesha kuwa mpango huo ni kama ulihujumiwa na baadhi ya waliochota fedha hizo kwani walizitumia kinyume cha makusudio na sasa ni kama Serikali imeshindwa kuzirejesha licha ya kumwajiri mkusanyaji kwa mwaka mzima.

Fedha hizo zilitakiwa kutumika kununulia malighafi, vyombo vya usafiri wa barabara, vifaa vya kilimo na ujenzi, wakati huo hali ya uchumi hususan ya upatikanaji wa fedha za kigeni ilikuwa mbaya, hivyo mpango huu ulikuwa usaidie kuinusuru hali hiyo.

Mwanzoni mwa 2011, Serikali iliingia mkataba wa mwaka mmoja na kampuni ya udalali ya Msolopa Investiment Limited ambayo kwa mujibu wa taarifa za uhakika, mkataba wake ulimalizika Januari mwaka jana bila kutimiza lengo la kurejesha mabilioni hayo.

Mkataba huo ulifikia ukomo huku Msolopa ikiwa imefanikiwa kukusanya kiasi cha Sh5 bilioni, sawa na asilimia 2.31 tu ya Sh216 bilioni ambazo bado zinadaiwa mikononi mwa wakopaji. Mkurugenzi wa Kampuni ya Msolopa, Ibrahim Msolopa alikataa kuzungumzia suala hilo akisema hana mamlaka...
“Mkataba wangu na Serikali juu ya suala hilo ulishafikia ukomo, nimeshakabidhi kila kitu kinachohusu CIS kwa Serikali kwa hiyo kama mnahitaji taarifa yoyote nendeni serikalini.”

Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa alisema halifahamu suala la watu kudaiwa fedha za CIS... “Ninahitaji muda wa kulifuatilia suala hili na kufahamu undani wake.”

Vigogo wanaodaiwa
Uchunguzi umebaini kuwa fedha hizo zimekaliwa na wafanyabiashara na wanasiasa kupitia kampuni zao wakiwamo wabunge wa CCM, Abbas Mtemvu (Temeke) na Henry Shekifu (Lushoto), Wenyeviti wa CCM wa mikoa, Ramadhan Madabida (Dar es Salaam) na Adam Kimbisa (Dodoma).

Kampuni ya Shamshi & Sons ya Shekifu ilikopa Yen za Kijapani 12,778,082.81 (sawa na Sh.207 milioni) kwa kuzingatia viwango vya sasa vya kubadilisha fedha ambavyo ni wastani wa Sh16.20 dhidi ya Yen moja.

Kampuni ya Cargo Plan International, ambayo mmiliki wake ni Kimbisa ilikopa Yen 2,882,961.79 (zaidi ya Sh46.7 milioni), wakati Tanzania Pharmaceutical inayomilikiwa na Madabida ilikopa Yen 7,031,983.29 (takriban Sh114 milioni).
Kampuni ya A.M.General Agency inayomilikiwa na Mtemvu ilikopa Yen 20,000,000 (sawa na Sh324 milioni). Taarifa zinaonyesha kuwa madeni hayo hayajalipwa.

‘KAGASHEKI JIUZULU’


Balozi Khamis Kagasheki

Dodoma. Kambi rasmi ya upinzani bungeni, imesema ni muda mwafaka kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki kujiuzulu kutokana na ama kwa kujua, au kutojua kuongoza njama za makusudi kutaka kumpatia mwekezaji wa Kampuni ya Otterlo Business Corporation (OBC) katika ardhi ya Loliondo.

Akiwasilisha maoni ya kambi hiyo kuhusu Makadirio ya Matumizi kwa mwaka 2013/14 ya Wizara ya Maliasili na Utalii juzi, Msemaji Mkuu wa kambi hiyo, Mchungaji Peter Msigwa alisema ardhi hiyo wanataka kuitoa kinyume cha sheria.“Huu ni wakati mwafaka kwa Waziri Kagasheki kuwajibika kwa kujiuzulu kwa hiari yake, au kama atashindwa kufanya hivyo, kuwajibishwa kwa kufukuzwa kazi kwa kusababisha mgogoro wa sasa maeneo ya Loliondo na Sale,” alisema.

Alitaka kujua kama ni kweli kitendo cha hivi karibuni cha Waziri Kagasheki kutoa amri ya wananchi wa Loliondo na Sale kunyang’anywa maeneo yao mengine na kukabidhiwa kwa Kampuni ya OBC, kilitokana na maagizo au maelekezo ya Rais Jakaya Kikwete.

Mchungaji Msigwa alisema kutokana na Kamati iliyoundwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kuchunguza mgogoro huo na kuongozwa na Naibu Katibu Mkuu CCM bara, Mwigulu Nchemba inaonyesha uamuzi huo ulikuwa uamuzi wake.

Hata hivyo, Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Songea Mjini, Dk Emmanuel Nchimbi aliilaumu kambi hiyo akisema inatoa kauli ya uongo ili hali ikijua ukweli kuhusu tuhuma dhidi ya Kinana.

Nchimbi alisema mmiliki wa meli ile anaitwa Bus Herman Ledley na walituhumiwa na kupelekwa mahakamani kwa kosa hilo kuwa ni pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya Team Fright (T) Ltd, Ladius Tesha, Gabriel Chambo wa Kampuni ya Import and Export Ltd, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Kigoma MN Enterprises Ltd, Shaaban Yasin Abdullah, mfanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bandari ya Dar es Salaam, Ericleo Morani, mfanyakazi wa Kampuni ya Kigoma MN Enterprises, Issa Ahmed Rwino na Mawakala wa Kampuni ya T Fright (T) Ltd, Nelbert Kiwale na Abubakar Omar Hassan.

CCM WAMGEUKA RC ARUSHA



WADAI AMEMWONGEZEA UMAARUFU LEMA, CHADEMA

VIGOGO wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwemo wabunge, wamemjia juu Mkuu wa Mkoa (RC) wa Arusha, Magessa Mulongo kwa jinsi alivyoshughulikia kesi ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA).

Wabunge hao waliliambia gazeti hili mjini Dodoma kuwa kesi ya uchochezi iliyofunguliwa na serikali dhidi ya Lema kwa shinikizo la mkuu huyo, itaiathiri kwa kiasi kikubwa CCM.

Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola alisema kuwa amefuatilia kwa makini chanzo cha kesi ya Lema na hatimaye kukamatwa na polisi mithili ya gaidi, na kubaini kuwa hulka za utendaji kazi wa baadhi ya viongozi wa serikali zinawapa sifa na umaarufu zaidi CHADEMA.

“Mimi sitaki kuingilia kesi, lakini ukiangalia kuanzia ile inayoitwa video ya vurugu za Chuo cha Uhasibu Arusha na jinsi Mkuu wa Mkoa alivyofika eneo la tukio na kuondoka, utabaini udhaifu mkubwa wa kiongozi huyo ambao leo unamfanya Lema aonekane shujaa.

“Leo tunaingia kwenye uchaguzi mdogo wa madiwani pale Arusha, tunaweza tukashinda, lakini tutafanya kazi ya ziada kwa sababu tu ya udhaifu wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha,” alisema Lugola.

Mbunge mwingine ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe, alisema alichokifanya Mulongo ni sehemu ya tatizo kubwa la viongozi wa serikali kujihusisha na ukereketwa wa kisiasa.

“Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa kuna kiongozi, tena hakumtaja jina, kwamba anapendwa kubebwa, alisema mwacheni abebwe. Alisema vile kuwazuia polisi kukabiliana na watu wanaopenda kumbeba kiongozi huyo.

“Mkuu wa Mkoa Arusha na wengine wanaokabiliana na wapinzani kwa nguvu kubwa bila sababu, hii inawaongezea umaarufu,” alisema mbunge huyo kutoka moja ya majimbo ya kanda ya kati.

Wednesday, May 1, 2013

CHADEMA YAUNGURUMA NA KUTEKA JIMBO LA MLALO HAPO JANA KATIKA MKUTANO WA HADHARA



Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema jana kilifunika katika uwanja wa Mnadani lukozi jimbo la Mlalo. Katika mkutano huo wananchi walitaja kero mbalimbai ikiwemo Ushuru mkubwa wa Ng"ombe kwa shilingi Elifu 6000, ngo'mbe ambapo wanapewa stakabadhi ya Sh 3000, Wananchi hao walihoji je huu si wizi? Kelvin aliwahoji na wakadia kwamba hawna tena imani na chama cha ccm na wamedai kwamba 2015 wa wananchi hataichgua tena.

Wananchi hao walilalamikia ushuru wa Mazao ambao ni Sh elfu 5 kwa gunia,
pia ujenzi wa soko la lukozi ambalo halijakamilika hadi Mda huu zaidi ya miaka 7 sasa.

Makamanda wa Chadema waliwahoji wanachi kama wanania na wana penda Mbunge ngirizi Arudi Madarakani wananchi walisema hawmtaki tena 2015 yeye na ndugu Lukas shemdolwa ambaye ni Diwani wa Kata ya Malindi lukozi jimbo la Mlalo. 

Wananchi wa Mlalo wamesema mbele ya makamanda we chadema kuwa hawamtaki Ngwirizi na ndugu lukasi shemdolwa na wamesema kitendo cha makada wa ccm kupiga risasi eneo hilo wiki tatu zilizopita ni utovu wa nizamu wa chama cha ccm, Kwani hakuna mwana ccm aliyekemea wala kulipoti tukio hilo Police hadi viongozi wa Chadema walipo kwenda kutoa riport polisi.

Wananchi wameapa kutowaamini tena viongozi wa ccm na wakachukua namba za simu za viongozi wa Chadema kwa ushrikiano zaidi, kwani viongozi waliowachagua wa ccm hawafai na ni wazembe.Wananchi wa Maeneo ya Mnadani Lukozi wamelaani sana tukio la 

Mtoto wa Mjumbe wa mkutano mkuu wa Taifa ccm ndugu Edmond Mdolwa, Mtoo wake Faustine Mdolwa kupiga Risasi wiki tatu zilizopita hap kijijini na kudai kwamba hakuna wa kumfanya kitu yeye ndie ccm.

WILLEM-ALEXANDER BECOMES NEW DUTCH KING



MUCH-LOVED BEATRIX ENDS REIGN DURING NATIONALLY TELEVISED SIGNING CEREMONY

Millions of Dutch people dressed in orange flocked to celebrations around the Netherlands Tuesday in honor of a once-in-a-generation milestone for the country's ruling House of Orange-Nassau: after a 33-year reign, Queen Beatrix abdicated in favor of her eldest son, Willem-Alexander. 

At 46, King Willem-Alexander is the youngest monarch in Europe and the first Dutch king in 123 years, since Willem III died in 1890. Like Beatrix before him, Willem-Alexander has assumed the throne at a time of social strains and economic malaise. 

Although the Dutch monarchy is largely ceremonial, he immediately staked out a course to preserve its relevance in the 21st century. 
Princess Beatrix of Netherlands, left, embraces her son, Dutch King Willem-Alexander and his wife Queen Maxima at the balcony of the Royal Palace in Amsterdam. 
 

"I want to establish ties, make connections and exemplify what unites us, the Dutch people," the freshly minted king said at a nationally televised investiture ceremony in Amsterdam's 600-year-old New Church, held before the combined houses of Dutch parliament. 

"As king, I can strengthen the bond of mutual trust between the people and their government, maintain our democracy and serve the public interest."
Hopes for the new monarch are high. For most of the 2000s, the country was locked in an intense national debate over the perceived failure of Muslim immigrants, mostly from North Africa, to integrate. In response, politicians curtailed many of the famed Dutch tolerance policies. 
 
More recently, this trading nation of 17 million has suffered back-to-back recessions. European Union figures released Tuesday showed Dutch unemployment spiking upward toward 6.4 per cent. That's below the EU average, but a 20-year high in the Netherlands. 

"Well, at least one person got a new job," she said.

"I am taking the job at a time when many in the kingdom feel vulnerable and uncertain," Willem-Alexander said. "Vulnerable in their work or health. Uncertain about their income or home environment." Amsterdam resident Inge Bosman, 38, said she doubted Willem-Alexander's investiture would give the country much of an employment boost.

MSIGWA AWALIPUA VIGOGO CCM, SERIKALI



WAZIRI NCHIMBI AJITOSA KUMSAFISHA KINANA

Mhe. Mch. Msigwa
MSEMAJI Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Mchungaji Peter Msigwa, amewalipua vigogo wa serikali na makada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), akidai kuwa wana maslahi yanayotilia shaka katika sekta ya uwindaji wa kitalii na kusababisha kuwapo kwa ujangili.

Kama alivyofanya mwaka jana na hata kwenye mikutano yake mingi ya hadhara, Msigwa alimtaja tena Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, na mkewe, kwamba anamiliki kampuni ya Sharaf Shipping Co, Ltd ambayo meli yake inadaiwa kunaswa na kontena la shehena ya meno ya tembo.

Hata hivyo, hotuba ya Msigwa ilikatizwa kwa mwongozo wa mbunge wa Viti Maalumu, Anna Abdallah (CCM), akihoji kitendo cha mbunge mwenzake kudai ofisi ya Spika ni kaburi la kuzika haki. Hata hivyo Spika Anna Makinda aliwataka wawe wavumilivu kwani yako maneno mengine mengi kama hayo.
Hata hivyo Msigwa aliendelea kusoma maoni ya kambi ya upinzani kuhusu makadirio ya matumizi na mapato ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka wa fedha wa 2013/14.

Huku wabunge wa CCM wakimwangalia kwa makini na wengine kutikisa vichwa kumpinga, Msigwa alimtaja mfanyabiashara na kada wa CCM, Mohsin Abdallah.

Msigwa ambaye alikuwa akikariri taarifa ya kamati ya waziri wa zamani wa wizara hiyo, Antony Diallo, aliwataja  makada waandamizi wengine wa CCM wenye maslahi ya aina hii kuwa ni kampuni ya Coastal Wilderness (Tz) Ltd., ambayo wakurugenzi wake wanatajwa kuwa ni Napono Edward Moringe Sokoine na Namelok Edward Moringe Sokoine; Enzagi Safaris (Tz) Ltd., yenye wakurugenzi Makongoro Nyerere, Muhamed Seif Khatib na Saidi Kawawa; na Hunting Safaris yenye wakurugenzi, Chande Kawawa na Hassan Kawawa.

Kampuni zingine ni M.S.K. Tours & Hunting Safari Co. ya Muhamed Seif Khatib.
Msigwa alisema mengi ya makampuni haya yalipewa vitalu vya uwindaji wakati hayana uzoefu wala mtaji wa kuendesha biashara ya uwindaji wa kitalii katika vitalu hivyo.

Alisema matokeo yake ni kwamba makampuni hayo yalishindwa kusimamia uhifadhi wa wanyamapori katika vitalu vyao na kusababisha tatizo la ujangili kushamiri katika vitalu hivyo.

“Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka serikali kutoa kauli mbele ya Bunge lako tukufu ni kwa nini serikali hii ya CCM imekuwa ikitoa vitalu vya uwindaji wa kitalii kwa makada waandamizi wa CCM ambao wanajulikana kuwa hawana weledi wala uwezo wa kibiashara wa kuendesha biashara ya uwindaji wa kitalii na hivyo kusababisha tatizo la ujangili kuwa kubwa zaidi na kuleta hasara kwa taifa letu!” alisema.

Akiwa amerejea bungeni baada ya adhabu ya siku tano, Msingwa alisema serikali imeanza kufedheheshwa katika mikutano ya kimataifa ya uhifadhi kwa sababu CCM imeamua kukumbatia makada wake waandamizi aliodai wanajihusisha na ujangili.

Alitolea mfano Mkutano wa 16 wa Nchi wanachama wa Mkataba wa Biashara ya Kimataifa ya Wanyama Walio Hatarini Kutoweka (CITES) uliofanyika Bangkok, nchini Thailand mwezi uliopita.

Bonyeza "Read More"