To Chat with me click here

Saturday, October 19, 2013

HIVI NDIVYO TEKNOLOJIA ILIVYO HIVI SASA!

Hii ni Kofia ya waendesha pikipiki ambayo inamwezesha mwendesha pikipiki kuona kwa nyumba bila kugeuza shingo wala kutumia vioo vya pembeni (side mirrors).

Flash Drive - hii ni ya kisasa kabisa, imetengezwa kwa GOLD na inauwezo mkubwa wa kutunza data zako. Uzuri wake zaidi ni kwamba ina lock-system, ambayo mtu hata akikuibia hataweza kuitumia labda awe anajua keyword yako.

Hiki ni chombo ambacho kinaweza kusaidia watu wengi ku-control matumizi yao ya vitu mbalimbali kama sukari, chumvi, n.k Kinauwezo wa kupima uzito au ujazo wa kitu kulingana na matumizi.

Friday, October 11, 2013

RWANDA DAY DRAWS CELEBRATIONS AND PROTESTS AGAINST PRESIDENT PAUL KAGAME



Rwandan-Canadians gathered in Toronto to connect with their community and learn about investment opportunities in their home country, as protesters loudly objected to the presence of President Paul Kagame.

Rwanda's President Paul Kagame

Hundreds of Rwandan-Canadians gathered in Toronto on Saturday to connect with their community and learn about investment opportunities in their home country.

But there was a small but noisy presence from a couple dozen protesters at the Rwanda Day event at Downsview Park, objecting to the presence of Rwanda’s controversial President Paul Kagame .

This was the first Rwanda Day held in Canada after previous versions in the U.S., London and Paris. Organizers said about 3,000 people attended, amid tight security and a large contingent of Toronto police.

“The main objective is to reconnect members of the community living abroad with their mother country,” said Shakilla Umutoni, Rwandan chargée d’affaires. That included updating them on developments in Rwanda and informing them of investment opportunities back home. 

About 15 Rwandan businesses and a few Canadian ones set up information booths at the event, she said, before the event turned into a party featuring a performance from Canadian rapper Shad, who was born in Kenya to Rwandan parents.

For Elvira Rwasamanzi, a 21-year-old biotech student from Ottawa, the focus on investing in Rwanda was one of the main draws of the day.
“It was really motivating,” said Rwasamanzi, who came to Canada from Rwanda as a young child. “It makes you want to give back because you’re proud.”

Kagame used part of his speech to encourage Rwandan-Canadians to invest in Rwanda, Umutoni said.
“He said if you travelled all the way from your country and got to Canada, take advantage of that . . . and do your best, not just for yourself but for your country.”

But it was the very presence of Kagame that brought protesters to the event, saying that Canada shouldn’t have let him enter given his record on human rights.

Rwandan opposition figures have been jailed and several countries suspended their aid to Rwanda last year citing its military support for M23 , a rebel group responsible for serious abuses in the Democratic Republic of Congo, according to the United Nations and human rights groups. Kagame has denied involvement.

Protesters also cited a 2010 UN report implicating the Rwandan government in killing tens of thousands of Hutus in the eastern part of what is now Congo, following the 1994 Rwandan genocide in which Hutus targeted Tutsis and up to a million people were killed. (Kagame and many of today’s government leaders are Tutsis.) Rwanda denounced the report. 

“Paul Kagame is a criminal financing a military movement in eastern Congo,” said Aime Kabuya of the Congolese Citizen Movement. “He shouldn’t have the freedom to travel that he does now. Why did Canada give him a visa?”

Perpétue Muramutse of the International Women’s Network for Democracy and Peace also raised concerns about Kagame’s pro-development message.

“The Rwandese are very poor,” she said. “They say there’s development in Rwanda but it’s development for just a small part of the people. When you go to the countryside, you see people with nothing to eat.”

Umutoni said she respected the right of protesters to express their views, but questioned why they were raising those concerns at Rwanda Day.
“This is purely a Rwandan event.”

Monday, October 7, 2013

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI




Ofisi ya Rais, Ikulu, imeanza mawasiliano na viongozi wa vyama vya siasa nchini vyenye hoja kuhusu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba uliopitishwa karibuni na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa nia ya kuandaa mkutano kati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wa vyama hivyo.

Mawasiliano hayo yameanza leo, Jumatatu, Oktoba 7, 2013, kufuatia maelekezo ya Rais Kikwete kwa Ofisi ya Katibu wa Rais.

Kufuatia matukio yaliyotokea Bungeni wakati wa kujadiliwa na kupitishwa kwa Muswada huo mwezi uliopita, na maneno na kauli mbali mbali ambazo zimetolewa na wabunge wa vyama vya upinzani na wadau wengine kufuatia kupitishwa kwa Muswada huo na Bunge, Rais Kikwete katika hotuba yake kwa wananchi Ijumaa iliyopita, Oktoba 4, 2013, alisema kuwa hoja na kauli za wanaopinga Muswada huo zinazungumzika kwa nia njema ya kutafuta mwafaka katika mchakato wa kutafuta Katiba Mpya.

Kwa mujibu wa maandalizi hayo, Ofisi ya Rais, Ikulu inaangalia uwezekano wa kuitisha mkutano huo Jumapili ya Oktoba 13 ama Jumanne ya Oktoba 15, mwaka huu.



Leo, Jumatatu, Oktoba 7, 2013, zimetungwa habari, zikaingizwa kwenye Mitandao ya Kijamii na kusambazwa sana zikidai kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametia saini Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ambao ulipitishwa na Bunge katika Kikao chake cha mwezi uliopita.

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu inapenda kufafanua kama ifuatavyo:

a) Kwanza, Ofisi ya Rais, Ikulu haijapokea Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Inawezekana Muswada huo umekwishakutumwa kutoka Bungeni lakini haujamfikia Mheshimiwa Rais. Hivyo, kama haujamfikia, Mhe. Rais hawezi akawa ameutia saini

b) Pili, Muswada huo ukimfikia Mheshimiwa Rais, inatarajiwa kuwa atautia saini kwa sababu Muswada huo umepitia katika mchakato sahihi na halali wa Kikatiba kwa maana ya kufikishwa Bungeni na Serikali, Kujadiliwa na hatimaye kupitishwa na Bunge.

c) Tatu, kama yapo marekebisho ambayo yanaonekana yanafaa kufanywa katika Sheria hiyo, basi yatafanywa na Bunge baada ya Mhe. Rais kuwa ametimiza matakwa ya Kikatiba ya kutia saini Muswada ambao umepitishwa na Bunge kwa kufuatia mchakato sahihi na halali wa Kikatiba.

d) Nne, na wala hii haitakuwa mara ya kwanza kwa Sheria kupitishwa na Bunge, ikatiwa saini na Mhe. Rais na baadaye kufanyiwa marekebisho na Bunge baada ya kuonekana umuhimu wa kufanya marekebisho hayo. Mwishoni mwa mwaka 2012, Sheria ya Marekebisho ya Katiba ilipitia njia hiyo.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.

7 Oktoba, 2013

VAN PERSIE AFURAHIA KUKUTANA NA MTU MKUBWA NA MREFU HASHEEM THABEET WA TANZANIA




Haijalishi kuwa anapokea mshahara wa pound 12.2 milioni kwa mwaka akiwa na Manchester United (Red Devils), lakini Robin Van Persie akikutana na Hasheem Thabeet, lazima aonekane mbilikimo. Na pia haijalishi kuwa, Van Persie ni mshambuliaji kwenye timu bora kabisa duniani, lakini akikutana na mchezaji mrefu zaaidi kwenye ligi ya NBA, Hasheem Thabeet wa Tanzania, lazima a-post picha Instagram na kuonesha kufurahi kwake. 

Wamarekani wanasema, “real recognize real” na ndio maana Van Persie amepost picha aliyopiga na Hasheem Thabeet. 

Hebu fikiria kwamba, kama picha hii angeipost Hasheem mwenyewe, isingekuwa big deal au sio? Lakini kwa kuwa imepostiwa na Van Persie mwenyewe, kaka hiyo ni kitu kingine. Kumbuka kuwa obama aliwahi kumwongelea Hasheem na sasa Van Persie, kwaweli ubora na umahiri wa Thabeet unaonekana wazi. Keep it up Dogo Hasheem Thabeet, na hongera sana.

Wednesday, October 2, 2013

WAZIRI MKUU ATAKA SOKO LA KAGUNGA LIKAMILISHWE


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma kuhakikisha kuwa anafuatilia suala la mkopo kwa ajili ya ujenzi wa soko la Kagunga hadi alikamilishe.

Ametoa agizo hilo jana jioni (Jumanne, Oktoba mosi, 2013) wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa kata ya Kagunga mara baada ya kuweka jiwe la msingi la soko la kimataifa la Kagunga ambalo liko umbali wa kilometa 1.5 kutoka mpakani mwa Tanzania na Burundi kwenye mwambao wa Ziwa Tanganyika.

Waziri Mkuu alisema kukamilika kwa ujenzi wa soko hilo kutatoa fursa za kibiashara baina wakazi wa kagunga na vijiji jirani pamoja na nchi ya Burundi ambayo milima yake inaonekana kutokea mahali soko lililojengwa. Mji wa karibu na Kagunga ni Nyanza Lac, ulioko kwenye jimbo la Makamba nchini Burundi.