Waziri Mkuu, Mizengo Pinda |
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amemtaka
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma kuhakikisha kuwa
anafuatilia suala la mkopo kwa ajili ya ujenzi wa soko la Kagunga hadi
alikamilishe.
Ametoa agizo hilo jana jioni (Jumanne,
Oktoba mosi, 2013) wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa kata ya Kagunga
mara baada ya kuweka jiwe la msingi la soko la kimataifa la Kagunga ambalo liko
umbali wa kilometa 1.5 kutoka mpakani mwa Tanzania na Burundi kwenye mwambao wa
Ziwa Tanganyika.
Waziri Mkuu alisema kukamilika kwa ujenzi
wa soko hilo kutatoa fursa za kibiashara baina wakazi wa kagunga na vijiji
jirani pamoja na nchi ya Burundi ambayo milima yake inaonekana kutokea mahali
soko lililojengwa. Mji wa karibu na Kagunga ni Nyanza Lac, ulioko kwenye jimbo
la Makamba nchini Burundi.
No comments:
Post a Comment