Haijalishi kuwa
anapokea mshahara wa pound 12.2 milioni
kwa mwaka akiwa na Manchester United (Red Devils), lakini Robin Van Persie akikutana na
Hasheem Thabeet, lazima aonekane mbilikimo. Na pia haijalishi kuwa, Van Persie
ni mshambuliaji kwenye timu bora kabisa duniani, lakini akikutana na mchezaji
mrefu zaaidi kwenye ligi ya NBA, Hasheem Thabeet wa Tanzania, lazima a-post
picha Instagram na kuonesha kufurahi kwake.
Wamarekani wanasema, “real
recognize real” na ndio maana Van Persie amepost picha aliyopiga na
Hasheem Thabeet.
Hebu fikiria kwamba,
kama picha hii angeipost Hasheem mwenyewe, isingekuwa big deal au sio? Lakini kwa
kuwa imepostiwa na Van Persie mwenyewe, kaka hiyo ni kitu kingine. Kumbuka kuwa
obama aliwahi kumwongelea Hasheem na sasa Van Persie, kwaweli ubora na umahiri
wa Thabeet unaonekana wazi. Keep it up Dogo Hasheem Thabeet, na hongera sana.
No comments:
Post a Comment