To Chat with me click here

Saturday, September 1, 2012

RAIS JAKAYA KIKWETE ATOA HESHIMA ZA MWISHO KWA MELES ZENAWI, ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO, AWEKA SHADA LA MAUA


Rais  Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kitabu cha maombolezo leo  ikulu ya Addis Ababa kufuatia kifo cha Waziri Mkuu wa Ethiopia Marehemu Meles Zenawi anayetarajiwa kuzikwa kesho. Wengine katika picha ni baadhi ya wajumbe waliofuatana na Rais Kikwete watakoshiriki mazishi ya kiongozi huyo.  Kutoka kushoto ni Mbunge wa Mtera Mhe.Livingstone Lusinde, Aliyewahi kuwa balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Jenerali Mirisho Sarakikya, Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Mhe.Joram Boswaro, Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe.Zitto Kabwe na Waziri wa Kazi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe.Haroun Ali Suleiman.
 Rais  Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua na kutoa heshima zake mwisho kwa aliyekuwa Waziri mkuu wa Ethiopia Marehemu Meles Zenawi katika Ikulu  ya Addis Ababa jioni hii
 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akito heshima zake mwisho kwa aliyekuwa Waziri mkuu wa Ethiopia Marehemu Meles Zenawi katika ikulu  ya Addis Ababa jioni hii
Rais Dkt.Jakaya Mrisho kikwete akikutana na kufanya mazungumzo na Kaimu Waziri MKuu wa Ethiopia Mhe. Hailemariam Dessalegn jijini Addis Ababa jioni hii.

RAIS KIKWETE AISHUKURU VODACOM KWA KUCHANGIA KATIKA MRADI WA KUHIFADHI MBWA MWITU HIFADHI YA TAIFA YA WANYAMA YA SERENGETI


Mtunzaji wa Mbwa Mwitu akiandaa mlo wa mwisho kwa wanyama hao 11 kabla hawajarejeshwa mbugani siku ya Alhamisi Agosti 30, 2012  baada ya kuhifadhiwa kwenye boma maalumu la mradi huo,  katika eneo la Nyamuma, Magharibi mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, mkoani Mara.
Mbwa mwitu hao wakijipatia mlo wao wa mwisho kabla ya kuachiliwa huru
 Ni vuta nikuvute
Mlo ukiendelea

PINDA - ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU KIKOTI MPANDA.


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kitoa heshima za mwisho kwa marehemu Mhashamu, Askofu Pascal William Kikoti katika ibada ya mazishi iliyofanyika kwenye kanisa kuu katoliki, jimbo la Mpanda, Septemba 1, 2012.

Mapadri wakiweka kaburini mwili wa aliyekuwa Askofu wa jimbo la Mpanda Mhashamu Pascal William Kikoti kaburini katika mazishi yaliyofanyika kwenye kanisa kuu la jimbo Katoliki la Mpada Mjini Mapanda Septemba 1, 2012

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitupa mchanga kwenye kaburi la Askofu Pascal William Kikoti katika mazishi yaliyofanyika kwenye Kanisa Kuu la Katoliki jimbo la Mpanda mjini Mpanda Septemba 1, 2012.

DK. SLAA: SITTA NI HATARI


ADAI NI MNAFIKI, MWONGO, NI KUTOKANA NA KAULI YAKE KWAMBA CHADEMA HAKINA VIONGOZI

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa amesema Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta ni mtu hatari ambaye CHADEMA kimegundua kuwa anaweza kufanya lolote kupata madaraka.

Dk. Slaa alisema Sitta hatakiwi kuaminiwa kwa kuwa hata alipokuwa spika, huku akiwa mwana CCM, mara kadhaa alijaribu kuomba kujiunga na CHADEMA iwapo CCM ingemtosa.

“Huyu mtu haaminiki hata katika dhamira yake, kwa kuwa tulikutana zaidi ya mara 100 na hata tukawa tunaandikiana vimemo, yeye akiwa katika kiti cha spika. Kama anabisha leo akanushe juu ya uhaini wake dhidi ya CCM,” alisisitiza Dk. Slaa.

Dk. Slaa alitoa kauli hiyo jana mjini Iringa wakati akizungumza na waandishi wa habari, akijibu kauli iliyotolewa na Sitta aliyedai kwamba CHADEMA hakijastahili kupewa madaraka kwa kuwa hakina watu wenye uzoefu wa uongozi.