Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) imetangaza majina ya wanafunzi
waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano kwa mwaka 2014 ambao waliomaliza
kidato cha nne mwaka 2013
Wanafunzi waliochaguliwa wanatakiwa kuripoti
kwenye shule walizopangiwa kuanzia tarehe 10 Julai 2014 na mwisho wa kuripoti
ni tarehe 30 Julai 2014.
Aidha, hakutakuwa na mabadiliko ya wanafunzi
kubadilishiwa shule walizopangiwa, hivyo wanafunzi wote wanatakiwa kuripoti
katika shule walizopangiwa kama inavyoonekana katika matokeo haya.
MAJINA
YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO MWAKA 2014
Maxmillian Kattikiro Blog inapenda kuwapongeza wanafunzi wote
waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na sita kwa mwaka 2014. Pia
tunapenda kuwatia moyo wale wote ambao hawakuchaguliwa kuwa, wasikate tama,
bado wanayo nafasi nzuri ya kurekebisha pale ambapo walitereza, na vilevile
watambue kuwa elimu haina mwisho.
No comments:
Post a Comment