ASKARI
Polisi, Mwashibanda Shibanda wa Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma, anadaiwa
kujihusisha na siasa za Chama Cha Mapinduzi (CCM), suala ambalo ni kinyume na
taratibu za jeshi.
Kwa
sasa Mwashibanda anasoma katika Chuo Kikuu cha Mzumbe, mkoani Morogoro, na
katika kipindi chote anadaiwa kufanya shughuli za kisiasa za wazi.
Mwashibanda
amepata kuwa mwenyekiti wa tawi maalumu la CCM Mzumbe, na mwenyekiti wa
shirikisho la matawi ya CCM mkoani Morogoro mwaka 2012 – 2013.
Mtoa
taarifa wetu amedokeza kuwa akiwa chuoni, anadaiwa kuwakamata wanachuo wenzake
kwa kushirikiana na polisi wa kituo cha Mzumbe, hasa wale wenye mirengo tofauti
na CCM.
Kwa
mujibu wa kumbukumbu mbalimbali za picha ambazo gazeti hili limeziona, askari
huyo anaonekana akiwa amevalia sare za CCM zenye rangi za njano na kijani akiwa
na makada na viongozi tofauti wa kitaifa.
Askari
huyo amewahi kuwa mkimbiza mwenge wa uhuru mwaka 2010 na akiwa mkoani
Shinyanga, alikaririwa akimpigia kampeni aliyekuwa mgombea urais wa CCM, Jakaya
Kikwete. Mwashibanda anatajwa kuzitia dosari mbio za mwenge baada ya
kuonyesha wazi kuipigia kampeni CCM wakati huo.
Kwa
mujibu wa vyanzo vyetu, askari huyo alifanya kituko hicho katika Kijiji cha
Wigelekelo, Shinyanga Vijijini wakati wa makabidhiano ya mwenge huo ukitokea
Manispaa ya Shinyanga.
Alisema
wilaya hiyo ni ya kihistoria, lakini imekuwa ikichanganywa na wanasiasa
wanaotangatanga kama kumbikumbi wasiokuwa na makazi.
“Watu
wa Maswa mtaonekana kuwa mmepotoka iwapo itaonekana mnampatia uongozi mtu
aliyejiunga na kanisa jipya, kwani huyo ana tamaa ya uongozi, hakuna
aliyezaliwa duniani kuwa kiongozi hadi kufa bali ni kuachiana zamu, sasa ni
zamu ya mwingine,” alisema.
Kauli
hiyo, ilionyesha wazi kumlenga Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda,
aliyejiondoa CCM na kuhamia CHADEMA baada ya kushindwa katika kura za maoni.
Hili
sio tukio la kwanza kwa askari kufanya siasa za wazi za CCM kwani katika
mkutano mkuu wa nane wa uchaguzi wa Umoja wa Vijana (UVCCM) Oktoba mwaka 2012 ,
mmoja wa wagombea wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Stanley Mdoe, alitiwa
mbaroni na polisi akibainika kuwa askari wa jeshi hilo.
Askari
huyo mwenye namba F 7961 wa cheo cha konstebo, alitoka Kituo cha Polisi
Mvomero, Morogoro.
No comments:
Post a Comment