Mhe. Zitto akiwa na mama yake mzazi B. Shida Salum enzi za uhai wake,kabla mauti kumkuta leo asubuhi katika hospitali ya AMI iliyopo Masaki,, jijini Dar Es Salaam. |
Aliyekuwa Mwenyekiti wa
Chama cha Walemavu Tanzania (CHAWATA), Bi Shida Salum, na Mjumbe wa kamati Kuu ya
chama cha CHADEMA, aliyekuwa amelazwa chumba cha Wagonjwa wanaohitaji uangalizi
maalum (ICU), katika Hospitali ya AMI, Masaki jijini Dar, ameaga Dunia.
Kwa habari zilizotufikia
katika vyombo vyetu vya habari, vimesema kuwa, mama wa Zitto alifariki leo
asubuhi katika hospitali hiyo ya AMI baada ya kulazwa hapo kwa muda ambapo
alikuwa akisumbuliwa na ungonjwa wa KANSA mpaka mauti ilipomkuta asubuhi ya
leo. Bi. Shida Salum, mbali na kuwa amekuwa akitibiwa AMI mpaka umauti ulipomkuta, lakini vilevile
amneshawahi kwenda kutibiwa ng’ambo ya nchi kama vile India bila mafaniko.
Habari hizi za kufariki kwa
mama yake Zitto zilielezwa na Zitto Kabwe mwenyewe kupitia mtandao wake wa
twitter, akiripoti kuondokewa na mzazi wake huyo.
Watu na baathi ya viongozi
mbalimbali wametoa salamu zao za rambi rambi kwa Mhe. Zitto kama ifuatavyo:-
Bernard
Membe:
Zitto Kabwe pole sana kwako
na ndugu kwa msiba huu mzito. Tunawaombea subira na Mwenyezi Mungu ailaze roho
yake mahali pema peponi, Amina.
William
Ngereja:
Nimepokea taarifa
za msiba wa Bi. Shida Salum (mama mzazi wa Zitto Zuberi Kabwe) kwa masiitiko
makubwa. Nawapa pole familia nzima ya ndugu yetu Zitto katika kipindi hiki cha
majonzi, Mwenyezi Mungu awape wepesi na pia, natoa pole kwa wote walioguswa na
msiba wa George Otieno aliyefariki jana, tuendelee kuziombea familia hizi na
nyingine zenye misiba ili wapate faraja kutoka kwa Mwenyezi Mungu ambaye ndiye
mfariji mkuu.
Maxmillian
Kattikiro (TEDA):
Napenda kuungana na wengine
wote walionitangulia kutoa salamu za pole kwa ndugu, rafiki, jamaa, kamanda na
mpambanaji mwenzutu, Mhe. Zitto Ruyagwa Kabwe pamoja na CHAMA CHA DEMOKRASIA NA
MAENDELEO (CHADEMA), kwa kuondokewa na Mama yake mzazi Bi. Shida Salum, na
mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA. Katika wakati huu mgumu na majonzi, tunakuombea
ili Mungu aendelee kukutia nguvu na kukuongoza vyema. Tunaungana nawe katika
kuomboleza msiba huu na Mwenyezi Mungu ampumzishe kwa amani mama yetu, Amina.
David Kafulila:
Nimepokea kwa huzuni kubwa
msiba wa mama yetu Bi Shida Salum. Ni mama mzazi wa zitto. Alinipenda sana na
nilikuwa karibu nae sana wakati wa uhai wake. Aliugua kwa muda kansa. Akapata
matibabu india kwa muda bila mafanikio sana na akaendelea kupata matibabu akiwa
Dar kupitia hospitali bora kabisa ya AMI. Nitambuka kwa ukaribu wangu kwake.
Alipenda kuwa karibu na mimi. Alikaa namimi mpaka usiku mwingi wa sanane
tunazungumza.alikuwa mama mcheshi, mwenye upeo na mwenye kufikiri kimkakati
siku zote. Alipenda kufunga na kusali. Nimepoteza kitu kikubwa kwa mama yetu
huyu. Mapenzi alokuwa nayo kwa watu wote. Naamini ametangulia kwa Mungu wa
upendo. Na hakika tutamkuta tufurahi nae pamoja siku moja.
Halima Mdee:
Pole sana
mh. Zitto kabwe, kwa kufiwa na mama yako mzazi Shida Salum,Najua hilo ni pigo kubwa katika maisha yako , lakini mungu amempenda zaidi, nakuomba uwe na moyo wa uvumilivu katika kipindi hiki kigumu, yote ni mipango ya Mungu, cha msingi ni kumuombea ili Mungu, aweze kumpokea mahari pema peponi amin. R.I.P Shida Salum.
No comments:
Post a Comment