To Chat with me click here

Friday, May 24, 2013

HAKUNA JAMII ITAKAYOACHWA NYUMA KIMAENDELEO: TANZANIA



Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Ramadhan Mwinyi, akizungumza wakati wa Mkutano wa 12 wa Masuala ya  Wazawa, kuhusu  mada ya utafiti uliofanywa kuhusu Ujasiri, Maarifa ya Jadi na Kujenga uwezo  Jamii ya Wafugaji katika Afrika. Nyuma ya Balozi ni  Bi. Ellen Maduhu Afisa wa Ubalozi .

Tanzania imesisitiza kwamba  inajukumu kubwa  la kuhakikisha kuwa mipango yake ya maendeleo endelevu inamfikia kila mwananchi na kwamba hakuna jamii itakayo achwa nyuma.

Na kwa sababu hiyo, Tanzania imeitaka  Jumuiya ya Kimataifa na wadau wengine kushirikiana na Serikali katika kufanikisha azma  yake hiyo, lakini pia kutambua  kuwa maamuzi mbalimbali inayoyachukua  yanafanyika kwa nia njema.

Hayo yameelezwa na   Balozi  Ramadhan Mwinyi, Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa   Tanzania katika Umoja wa Mataifa,  alipokuwa  akichangia  majadiliano ya mada   ya utafiti kuhusu Ujasiri, Maarifa ya Jadi na Kujenga Uwezo wa Jamii ya  Wafugaji katika Afrika.

Mada  hiyo ni sehemu ya mada kadhaa zikiwa zao afya, elimu, haki za binadamu, ujasiliamali, vijana mila na tamadu  ambazo zimekuwa zikijadiliwa kwa nyakati tofauti  katika Mkutano wa Kudumu  wa  12  Kuhusu Masuala ya Wazawa. ( Forum on   Indigenous Issues) Mkutano huu ambao ulianza mapema wiki hii  unafanyika chini ya  usimamizi wa  Baraza la Uchumi na Maendeleo ya Jamii la Umoja wa Mataifa ( ECOSOC).

Washiriki wa  mkutano  huu   wapatao  2000   wanatoka katika  Asasi zisizo za kiserikali  wakiwamo wawakilishi kutoka   baadhi ya  taasisi za kifedha kama  Banki ya Dunia,  Banki ya Maendeleo ya Afrika  na  Banki  ya Maendeleo ya Asia.

“Tunaendelea na  jitihada  za kuwaletea maendeleo wananchi wetu ili kuhakikisha kwamba hakuna jamii inayoachwa nyuma  kama ambavyo imeainishwa katika Malengo ya Maendeleo ya Millenia ( MDGs) na  kutafsriwa katika Mpango wa Maendeleo ya Taifa na   mipango  migineyo” akasisitiza Balozi Mwinyi.

Hata hivyo akasema licha ya jitihada hizo za serikali , bado kuna baadhi ya jamii chache ambazo zenyewe zimeamua    kudumisha  mila, tamaduni na   maisha yao ya jadi .

Akasema  jamii hizo ni zile ambazo hazifahamiki  sana katika Jumuiya ya Kimataifa kama ilivyo kwa jamii ya  wamasaai.

Akizungumzia  masuala ya upatikanaji  na ugawaji wa ardhi kwa wananchi  zikiwamo   jamii ambazo mfumo wa maisha yao unategemea zaidi ardhi na mali asili nyingine. Balozi   Mwinyi amewaeleza washiriki  wa  mkutano huo wakiwamo washiriki kutoka Tanzania, kwamba serikali imejiwekea sheria na taratibu zinazosimamia ugawaji wa ardhi.

Akafafanua  kwa kueleza kwamba kwa sheria na taratibu za Tanzania,   Hati ya umiliki wa Ardhi katika  ngazi ya kijiji hutolewa  kwa wanajamii ambao wanaishi au wamekusanyika katika  muundo wa kijiji ambao unatambuliwa rasmi.

“ Kwa mujibu wa sheria zetu, ni kijiji  ndicho  kinatambuliwa kisheria  kama chombo huru kinachosimamia masuala ya ardhi ambapo cheti  cha ardhi hutolewa kwaajili ya matumizi ya jamii nzima”. Akasema

Na kuongea “ Hata hivyo    kuna  baadhi ya maeneo  hasa yale ya wawindaji ambapo kama idadi ya  jamii ile haikukidhi  matakwa ya kisheria ya kuwa na hadhi ya kijiji kutokana na uchache wao, bado kwa mfano,  mwaka 2011, serikali ilitoa  hati ya  kumiliki ardhi kwa  ya Wahdzabe ingawa walikosa sifa  zinazotakiwa kisheria.

Akizungumza kuhusu  Loliondo ambako  Serikali imetangaza kutenga eneo la kiasi cha kilomita za mraba 2,500  za ardhi kwaajili ya  makazi ya jamii ya wamasaai  na ambao wengi wao hawakuwa na ardhi na hivyo kuwa katika mazingira magumu. Balozi amesisitiza kwamba uamuzi huo ulikuwa ni wa manufaa kwa jamii hiyo na taifa kwa ujumla.

Akasema kuwa  eneo  lililotengwa   ni kubwa  kuliko nchi ya Luxeburg au  mara nne ya eneo la nchi ya Singapore ambayo ina kilomita za mraba 624.

Akasema eneo  lililobaki la kilomita za mraba 1,500 Serikali imelitenga kwaajili ya hifadhi ya wanyama pori na mazalia yake ikiwa ni  pamoja na uhifadhi wa uoto wa asili, utunzaji wa vyanzo vya maji  kwa maendeleo endelevu ya  uwepo wa wanyama na kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Naibu Mwakilishi wa Kudumu akafafanua Zaidi kwa kueleza kwamba, uamuzi huu wa Serikali wa kutenga ardhi kwaajili ya matumizi ya  binadamu  na mengine  kwa hifadhi ya  maliasili ni uamuzi halali na wala haukuanza sasa  bali umekuwa  ukitekelezwa katika  maeneo mengi ya nchi tangu uhuru.

NA MWANDISHI MAALUM, NEW YORK

KENYATTA ATAJA MAWAZIRI WAWILI WA MWISHO


Rais Kenyatta.

Raisi wa Kenya Uhuru Kenyatta siku ya Alhamisi (tarehe 23 Mei) alitoa majina mawili ya mwisho ya baraza lake la mawaziri lenye wajumbe 18, mwezi mmoja tangu mchakato wa uteuzi kuanza. 

Meneja wa hoteli ya Utalii Joseph Ole Lenku ameteuliwa kwa nafasi ya mambo ya ndani na uratibu wa serikali ya kitaifa, na mbunge wa zamani Samuel Kazungu Kambi kuwa waziri wa kazi, usalama wa jamii na huduma. 

"Hatimaye nimeshapeleka majina bungeni kwa ajili ya kuthibitishwa," Kenyatta alisema, kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation la Kenya. 

Kamati ya bunge ya uteuzi itawachunguza wawili hao na kupeleka ripoti kwa Bunge la Taifa. 

Uteuzi wa Lenku na Kambi unakuja wiki moja baada ya bunge kupitisha wajumbe wa baraza la mawaziri waliobakia na kuwaapisha kwa ajili ya nafasi zao.

WAMEMDHARAU NYERERE NA KUIVUNJA MISINGI - SASA HAWANA PA KUSHIKILIA!



Kwao Nyerere siyo "Baba wa Taifa" tena; kwao ni "Mzee Nyerere"; kwa watawala wetu hawa walioshindwa wanasema wamefanya mambo mengi sana ya maendeleo kkuliko "Wakati wa Nyerere". Wanajitamba kuwa wao wamekuza sana demokrasia na kuwa hata "Nyerere" hakuweza kufanya waliofanya wao. Katika upotofu wao wanaamini kabisa kuwa wao wanapendwa zaidi; na wanapendwa kwa sababu wamefanya mengi mno na hawaelewi kwanini watu hawaoneshi shukrani! 

Ndio maana kila kukicha hawaachi kubembeleza kwa wananchi kuwa "hamuoni tunayofanya" na kuwa watu wanalaumu tu lakini hawatoi pongezi kwa "mazuri mengi". Imefika mahali Kikwete mwenyewe amedai mahali fulani anataka kukumbukwa kuwa ni "bwana maendeleo"; anasema hivi kwa sababu anapokaa ofisini anaamini kabisa kuwa ameweza kuwapatia Watanzania 'vitu" vingi sana vya maendeleo kuliko wakati wowote wa historia - vitu ambavyo hata Nyerere hakuweza kuwapatia. Kikwete anataka awe juu ya Nyerere kwa kila kipimo kwani kipimo kilichowekwa ni Nyerere. Na bila ya shaka kuna sababu - Nyerere hakuamini kuwa walikuwa tayari kuwaongoza Watanzania - hawa kina Kikwete na Lowassa. 

Sasa katika kumdunisha Nyerere ili wao wakue wameacha propaganda chafu dhidi ya Nyerere na uongozi wake. Leo hii tunashuhudia mambo ambayo - pamoja na 'ubaya' wote wa Nyerere hayakuwahi kutokea chini ya "dhaalim Nyerere"! Matukio yanayotokea leo hii ukiwaambia watu walioshi wakati wa Nyerere, chini ya chama kimoja na uongozi thabiti hawawezi kuelewa yanawezekana vipi kutokea. Watu wa enzi za Mwalimu wanakumbuka vizuri kuwa kiongozi aliyefanya madudu hakuvumuliwa; na bahati mbaya wakati ule hatukuwa na wasomi wengi na watu wengi wenye udhoefu lakini Nyerere hakuwaonea huruma. Wapo ambao hadi leo wana kinyongo na Nyerere kwa sababu hakuwapa nafasi nyingine. 

Lakini katika kumdharaulisha Nyerere na kujaribu kupuuza mafanikio yake makubwa zaidi wamejikuta hawana pa kukimbilia! Tuliokuwa wakati wa Nyerere hatukumbuki jinsi JWTZ likitumiwa kisiasa kama linavyotumika hivi sasa! Fikiria ndege ya jeshi itumwe kumchukua raia kumpeleka Mahakamani!? Kwamba, ati vurugu za uchaguzi zilazimishe JWTZ kuingilia kati! Kwamba vikosi vya kutuliza ghasia vya polisi vizidiwe nguvu na mara moja kuliingiza jeshi kufanya kazi za jeshi la polisi! Unthinkable! Lakini wao wanaamini wako sawa! 

Lakini siyo kwamba wamedharaulisha na kumtupa nje Nyerere ni zaidi ya hivyo; wameitupa misingi ya taifa letu. Wanataka kujenga kwa misingi ya mabua! Waliachiwa misingi ya zege lakini wao wakiamini ni 'magenius" wameamua kutengeneza 'taifa jipya' nje ya misingi iliyounda Tanzania. Leo hii Watanzania kwa mamilioni wananung'unika moyoni kwani hawatambui kama hili ndilo Taifa waliloachiwa kama urithi. Sasa hivi inaonekana Tanzania inazidi kufanana zaidi na mataifa mengine ya Afrika kiasi kwamba linaweza lisitofautike tena mbele ya umma. 

Wameitupa misingi sasa hawana cha kujengea; wamebakia kutumainia vitisho, dharau na matumizi ya nguvu. Wameshindwa kabisa kujenga hoja - kwa mfano kwenye hili suala la gesi. Hawana ushawishi wa hoja na badala yake hata kauli zao wanazotoa zimejaa dharau (contempt) na matokeo yake watu nao wanawadharau! Wanafikiri vitisho na kejeli zinajibu hoja! 

Kushindwa kwa sera zao mbalimbali ni matokeo ya kuachana na misingi ya taifa; wanafikiri wanaweza kutengeneza sera nzuri nje ya misingi ya taifa! Matokeo yake: 

  • Sera ya Nishati na Madini imeshindwa
  • Sera yao ya Gesi imeshindwa - hata kabla haijaanza!
  • Sera yao ya Elimu imeshindwa
  • Sera yao ya siasa imeshindwa
  • Sera yao ya Sayansi na Teknolojia imeshindwa 
  • Sera yao Mazingira imeshindwa 

N.k

Wameshindwa lakini hawaamini wameshindwa na badala yake wanawalaumu wanaowaambia wameshindwa kwa kushindwa kwao! Kana kwamba, wanaowalaumu wakinyamaza basi wao wataweza! Wenyewe wanaambizana kuwa wakipewa nafasi nyingine 2015 basi wataaanza kuweza; na wapo watu wanaamini kuwa hilo linawezekana; kwamba pundamilia anaweza kugeuka na kuwa farasi! Kama wenyewe wameshindwa kuvuana magembe licha ya mbwembwe zote za "kuvuana magamba" kweli kuna uwezekanow wataweza? Na ukweli ni kuwa walipofika sasa hawawezi kurudi kwenye misingi ya Nyerere na Taifa letu; kwa sababu kurudia misingi hiyo ni kujishtaki katika historia.

kuna namna moja ttu ya kuwasaidia... kuendelea kuwakataa.

Maskini CCM!
Maskini Kikwete
Maskini Tanzania chini yao!

DK. SLAA: MTWARA WAMEPUUZWA


Dr. Slaa

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amesema Rais Jakaya Kikwete anapaswa kuomba hekima kwa Mwenyezi Mungu kutokana na matukio yanayotokea sasa nchini.

Alisema hali inayotokea sasa ni matokeo ya wananchi kupuuzwa na kutokusikilizwa katika suala zima la uwekezaji unaofanyika sehemu mbalimbali za nchi.

Dk. Slaa alitoa kauli hiyo jana katika kijiji cha Giroda Babati vijijini, wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika ziara yake ya siku tisa ya ujenzi wa Chama mkoani Manyara.

Kabla ya kutoa kauli hiyo Dk. Slaa aliwaomba wananchi wasimame kwa muda wa dakika moja, kuomboleza vifo vilivyotokea mkoani Mtwara. Aliongeza kuwa kuendelea kuwapuuza wananchi wa Mtwara ni kuendelea kucheza na jipu linalopaswa kutumbuliwa na kwamba njia sahihi ni kukaa na kuwasililiza wananchi katika uwekezaji na kufikia muafaka pasipo kutumia nguvu.

Alisema wanachotaka wananchi wa Mtwara ni kujua namna watakavyonufaika kwa kile alichoeleza kuwa katika uwekezaji wowote wanufaikaji wa kwanza wanapaswa kuwa wananchi. Alisisitiza kuwa katika hali ya Mtwara kulihitajika busara za kawaida za kutatua msingi wa tatizo badala ya wananchi kupigwa mabomu, risasi na kisha kukamatwa.

“Ni jambo la aibu kuwapiga mabomu wananchi wanaodai kunufaika na rasilimali za nchi yao hapa kunahitajika elimu ya kuwafahamisha haki zao ni zipi na siyo mabomu,” alisema Slaa.

Wednesday, May 22, 2013

EGYPTIAN PRESIDENT ANNOUNCES RELEASE OF OFFICERS KIDNAPPED IN SINAI


President Mohamed Morsi

CAIRO — President Mohamed Morsi on Wednesday (Today) announced the release of seven Egyptian security officers who had been kidnapped nearly a week ago in the lawless Sinai Desert, ending days of mounting anxiety over the government’s apparent inability to secure even its own soldiers and police in the area. 

The persistent lawlessness of Sinai since the Egyptian revolution has become an international concern because the region borders Israel and the Hamas-controlled Gaza Strip, and this week a strike by police officers angry at the kidnapping had closed police stations and border crossings around the area. The crisis recalled an attack on a Sinai military checkpoint last August that resulted in the deaths of 16 soldiers, humiliated the Egyptian military, and helped compel the generals who had ruled Egypt to hand full power to the first civilian president, Mr. Morsi. 

The president’s announcement, however, shed no light on the identity of the abductors or the explanation for the release. There was no mention of any arrests or punishment for the kidnapping. The captives — one soldier and six police officers — were left in a remote stretch of desert and retrieved by a military helicopter. 

Mr. Morsi vowed in a brief speech that “the criminals responsible for such incidents must be held accountable. There’s no backing down in that.” He added: “Those who have rights must get them, but the law rules everywhere.”
But at times he sounded almost plaintive. He pleaded with the residents of Sinai to disarm. “I call on everybody in Sinai who has weapons to give up their weapons,” Mr. Morsi said. “The homeland is bigger than all of us and weapons should only be with the authorities, with the men of the armed forces and the Ministry of Interior,” he continued, pledging to uphold public security and asking those with grievances to express them peacefully. 

LOWASSA KAMA RAIS ITAKUWA NI KIKWETE 2.0 (MARUDIO YA 2005)




Hawajakutana mtaani; wametoka mbali, na inajulikana kwa wengi kuwa safari yao kuelekea Magogoni ilikuwa na ahadi baina yao kuanzia 1995. Ushirika wao au Ubia wa uongozi wao ulikuwa wazi kuwa yeyote kati yao angeteuliwa kuwa Rais basi mwenzie angekuwa Waziri Mkuu. Matokeo yake Katiba ilifanyiwa mabadiliko 2005 ili kuhakikisha kuwa Waziri Mkuu anakuwa mtu wa tatu kuushika Urais katika Mnyororo wa Kufuatana kiuongozi (Rais, Makamu wa Rais halafu Waziri Mkuu). Kabla yake wa tatu kiuongozi alikuwa ni Spika. Bila ya mabadiliko yale Spika Sitta angekuwa anakaiumu Urais wakati wowote RAis na Makamu hawapo nchini.

Kashfa ya Richmond kama alivyosema Kikwete mbele ya wazee wa Dar ilikuwa ni "ajali ya kisiasa" tu kwa Lowassa. Ilikuwa ni ajali mbaya hata hivyo kwa sababu ilivuruga kwa kiasi kikubwa na imeacha ombwe kubwa sana la kujijenga tena Lowassa. Lakini halikufuta ndoto ya yeye kuutaka Urais; wengine wanaweza kusema ni "haki" yake; aliahidiwa kupokezana; anatoka Kikwete anaingia Lowassa.

Je, utawala wa Lowassa unaweza kuwa tofauti? Well, je nyani akiamua kuondoka shambani na kuwaachia ngedele mahindi yatakuwa salama? Kufikiria kuwa CCM chini ya Lowassa na Tanzania chini ya Lowassa itakuwa tofauti ni kujaribu kukinga mikono jangwani kungojea mvua.

Kwa ufupi, yeyote anayetaka mwendelezo wa utawala wa Kikwete kwa miaka kumi ijayo - ndani ya CCM na kwa taifa - uchaguzi uko wazi - kuhakikisha kuwa Lowassa anachaguliwa kuwa Rais. AU watu watuambie utawala wa Lowassa utakuwa na tofauti gani na utawala wa Kikwete na kwanini?
Lowassa na Jk ni watu wanaofanana kimvuto machoni mwa watu.Kama ni kwa mganga wa kienyeji watakuwa walikwenda kwa mganga mmoja.hata kiutendaji ni watu ambao hawatofautiani sana.Watu wengi walimchaguwa Jk kutokana na mvuto aliokuwa nao kwa watu pia na jinsi alivyo waaminisha watanzania kuwa ndiye mwenye uwezo wa kuwaletea maisha bora watanzania.Maisha bora ambayo yameshindikana kabisa.Lowassa naye pamoja na kuwa na mvuto kwa watu naye anajinasibu kama mtu mwenye kuthubutu mwenye maamzi magumu kauli ambayo imepondwa na Magufuli kuwa anae toa maamzi magumu ni kibaka Rais anatoa maamzi makini.Maneno yote ya kuthubutu na maamzi magumu ambayo lowassa anajaribu kuwaaminisha watz ili wamuone kuwa ndiye mtu pekee ambae anaweza kuwaletea mabadiliko watz lakini hakuna mabadiliko yoyote ambayo anaweza kuyaleta tofauti na Jk.ukizingatia kuwa alikuwa na nafasi kubwa sana serekalini nafasi ambayo angeweza kuitumia kuleta mabadiliko ambayo anajaribu kuwaaminisha watz waamini kuwa anaweza kuwaletea endapo watamfanya kiongozi wao kwa mara nyingine tena.