To Chat with me click here
Showing posts with label ESCROW. Show all posts
Showing posts with label ESCROW. Show all posts

Monday, December 29, 2014

TEC ‘POWERLESS’ ON KILAINI, NZIGILWA



Pope Francis
Dar es Salaam. Only the Pope can determine the fate of two senior Catholic clergymen said to have received part of the Sh306 billion withdrawn from the Tegeta escrow account,  according to Tanzania Episcopal Conference (TEC) vice president Severin Niwemugizi.

Speaking to the sources of this news from Ngara yesterday, Bishop Niwemugizi dismissed reports that Methodius Kilaini and Eusebius Nzigilwa, the auxiliary bishops of Bukoba and Dar es Salaam, respectively, had been summoned for questioning. He added that TEC had not and would not  summon any religious leader for questioning over the matter.

“As a senior TEC leader, I can confirm that no one has been summoned for questioning so far and we don’t intend to do so.

“It’s only the Pope who has the authority to summon bishops....I wish to make it clear that there is no provision in the Roman Catholic system in this country that provides for the summoning of bishops for questioning.  TEC does not have such powers, which rest with the Vatican,” said Bishop Niwemugizi, who heads the Rulenge-Ngara Diocese.

Bishop Kilaini and Bishop Nzigilwa  received Sh80 million and Sh40 million, respectively, from Mr James Rugemalira, a former shareholder in Independent Power Tanzania Limited.  The money was transferred to the bishops’ accounts at Mkombozi Commercial Bank, which is operated by the Catholic Church.

Bishop Niwemugizi said the Vatican only launched disciplinary proceedings upon satisfying itself that a bishop had committed a serious transgression.
However, he could not say whether the Vatican had information about the two Tanzanian bishops.

“I don’t know if the Pope is aware of this matter.  As you are aware, I’m in Ngara and the Pope is in Rome,” he said. Bishop Nzigilwa declined to comment on the matter after leading Christmas Mass at St Joseph’s Cathedral in Dar es Salaam last Thursday.
 
“We are celebrating Christmas...let’s stick to this as I prepare an explanation about the issue you are interested in. I will give it to you once it is ready,” he said.

The two bishops were among a number of people named in Parliament as beneficiaries of the escrow account money.
Others include Prof Anna Tibaijuka, who was sacked earlier this month by President Jakaya Kikwete, who said there were ethical questions after Sh1.6 billion was transferred to the personal account of the former minister of Lands, Housing and Human Settlements Development.

Mr Frederick Werema resigned as Attorney General on December 16, saying his advice to the government regarding the transfer of IPTL ownership was “misunderstood”.

Energy and Minerals Permanent Secretary Eliakim Maswi was suspended last week pending a new investigation into his role in the controversy.
The escrow account saga dominated Christmas sermons last week.

Saturday, December 27, 2014

WALIOPATA MGAWO ESCROW KUTOZWA MAMILIONI



Dar es Salaam. Watu waliopokea mgawo wa fedha zilizochotwa kutoka katika Akaunti ya Tegeta Escrow ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) huenda wakalazimika kulipa mamilioni ya Shilingi ambayo ni kodi ya mapato ya fedha walizopewa, imefahamika.

Hata hivyo, habari zinasema malipo hayo ya kodi yatafanywa kwa kuzingatia matokeo ya uchunguzi wa vyombo vya dola ambao unawashirikisha maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhusu uhalali wa fedha walizolipwa.

Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba alisema juzi kuwa wote waliopokea mgawo wa fedha zilizochotwa kutoka katika akaunti hiyo watapewa fomu za kuthibitisha mapato yao ili wakatwe kodi kutokana na fedha hizo ambazo pia zinapaswa kuhakikiwa na vyombo vya usalama kwamba ni mapato halali.

Alisema taratibu za kufuatilia fedha hizo zimekwishaanza na ifikapo Desemba 31 wahusika watapewa fomu ili kuthibitisha mapato yao ili hatua za kuwatoza kodi zianze.

Askofu Eusebius Nzigirwa
Msingi wa maelezo ya Nchemba umejengwa kwenye Sheria ya Mapato ya Kodi (Income Tax Act) ya 2012 ambayo inaelekeza mlipaji wa kodi kuwasilisha ankara za hesabu za mapato yake kwa TRA kila ifikapo mwisho wa mwaka na hesabu hizo huiwezesha mamlaka hiyo kutathmini kiwango cha kodi inayopaswa kulipwa na mhusika.

“Hotuba ya Rais (Jakaya Kikwete) imetupa nguvu kuendelea na juhudi ambazo tayari tulikwishazianza tangu awali, maana amesisitiza kwamba lazima kodi ilipwe na sisi hilo ni jukumu letu, tutafuatilia ili kuhakikisha kwamba fedha za walipakodi zinarejeshwa,” alisema Nchemba.

Ikiwa wote waliotajwa watalazimika kukatwa asilimia 30 ya fedha walizopewa kama kodi ya mapato, TRA itakusanya zaidi ya Sh9.3 bilioni ambazo zinatokana na karibu Sh31 bilioni zilizotawanywa kwa watu na kampuni mbalimbali kutoka kwenye akaunti ya mmiliki wa VIP Engineering, James Rugemalira.

Askofu Methodius Kilaini
Miongoni mwa waliokiri kupokea fedha hizo ni aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka ambaye alipata mgawo wa Sh1.6 bilioni akisema fedha hizo zilikuwa ni za mchango wa kulipa mkopo wa shule anayoisimamia.

Hata hivyo, hatua yake hiyo tayari imemgharimu baada ya Rais Jakaya Kikwete kutengua uwaziri wake kutokana na kile alichokiita kuwapo kwa makosa ya kimaadili hasa ikizingatiwa kuwa fedha hizo ziliingizwa kwenye akaunti yake binafsi.

Taarifa ya PAC
Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) ikiwasilisha taarifa yake bungeni kuhusu suala hilo mwezi uliopita, pia iliwataja wengine waliochukua fedha hizo kutoka VIP Engineering kuwa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti na Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge (Sh1.6 bilioni), aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini ambaye pia ni mbunge wa Sengerema, William Ngeleja (Sh40.4 milioni) na Mbunge mstaafu wa Sumbawanga (CCM), Paul Kimiti (Sh40.4 milioni).

Jaji Aloysius K Mujulizi
Wengine ni aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona (Sh40.4 milioni), aliyekuwa mjumbe wa Bodi ya Tanesco, Dk Enos Bukuku (Sh161.7 milioni), Majaji wa Mahakama Kuu, Profesa Eudes Ruhangisa (Sh404.25 milioni) na Jaji Aloysius K Mujulizi (Sh40.4 milioni) pamoja na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usajili wa Vizazi na Vifo (Rita), Philip Saliboko (Sh40.4 milioni).

Pia wamo aliyekuwa Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji (TIC), Emmanuel Daniel Ole Naiko (Sh40.4 milioni), Ofisa wa TRA, Lucy Appollo (Sh80.8 milioni), Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba, Methodius Kilaini (Sh80.9 milioni), Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Eusebius Nzigirwa (Sh40.4 milioni) na Padri Alphonce Twimannye Simon (Sh40.4 milioni).

Wednesday, December 24, 2014

UTOUH: ZA EPA ZILIRUDI, ZA ESCROW ZIRUDI!


Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
(CAG) mstaafu,Ludovick Utouh

MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) mstaafu, Ludovick Utouh, amesema serikali inatakiwa kuhakikisha fedha zake zilizokuwepo kwenye akaunti ya Tegeta Escrow zinarudi kama ilivyokuwa kwa zile za EPA.
Katika mahojiano yake na Raia Mwema yaliyofanyika jijini Dar es Salaam wiki hii, Utouh alisema kama angepewa fursa ya kumshauri Rais Jakaya Kikwete kuhusu nini cha kufanya na suala la Escrow bila shaka angemwambia ahakikishe anapata kwanza fedha zilizopotea.
“Kwanza niseme kwamba aliyetoa pendekezo kwa serikali kwamba iwabane walioiba fedha za EPA wazirudishe kwanza kabla ya kufuata mikondo ya kisheria ni mimi. Hela kurudi ni jambo la muhimu sana.
“Ushauri wangu ni kwamba uchunguzi unatakiwa ufanyike na wale watakaobainika kufanya wizi basi warudishe fedha walizoiba na halafu wapelekwe mahakamani.
“Watu wanaolalamika kuhusu wezi wa EPA wanafanya hivyo kana kwamba watu walirudisha fedha na wakaachiwa jambo ambalo si la kweli. Hela zilirudi na bado kesi zikaendelea mahakamani na zinaendelea hadi hivi leo tunavyozungumza.
“Hivi kuna tatizo gani kama mtu atarejesha fedha aliyochukua? Huyu mtu unaweza kumkuta na hatia na ukampeleka jela lakini akifika kule atakula na kulala bure kwa gharama za walipa kodi. Kama atalipa fedha alizoiba, ndizo fedha hizohizo zitatumika kumhudumia.
“Ninachosema hapa, kitu kizuri ni kipi? Kuendelea na kesi kwa miaka mingi na huku ukitumia fedha za umma kuzihudumia au angalau kushinikiza kwanza hela zilizochukuliwa zirudishwe na kesi zikaendelea kama kawaida?
“Kutaka hela zirudishwe haina maana hata kidogo ya kusamehe watuhumiwa bali maana yake ni kuhakikisha kile kilichochukuliwa kinapatikana kwanza,” alisema Utouh.
Katika mahojiano hayo, Utouh alisema ni sahihi kwa ripoti ya CAG kuhusu suala la Escrow kusema fedha zilizokuwepo katika akaunti ya Escrow ni za umma na pia si umma kwa vile huo ndiyo ukweli.
“Kama ulifuatilia mjadala ule wa bungeni, kitu cha kwanza ambacho kilisemwa na kipo kweli ni suala la kodi. Ndani ya fedha zilizokuwepo kwenye akaunti ya Escrow kulikuwa na kodi. Kodi ni mali ya umma. Hivyo kwenye eneo hilo la kodi, fedha za umma zipo.
“Jambo la pili lipo kwenye historia ya kuanzishwa kwa akaunti hiyo. IPTL na Tanesco walikuwa na mzozo kuhusu malipo ya capacity charge. Mgogoro ulikuwa mkubwa na wakaamua kuweka fedha za malipo hayo kwenye akaunti ya Escrow huku wakisubiri shauri lao kutoka katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro.
“Sasa, nizungumze kama mfano tu, hypothetical, kwamba IPTL walikuwa wanaichaji Tanesco shilingi 30 kwa siku. Tanesco wakaona kwamba wanalaliwa kwa gharama hizo. Wanalipa zaidi ya wanavyotakiwa kulipa.
“Wakaenda mahakamani kushitaki. Uamuzi uliotoka ni kwamba, ni kweli Tanesco wamebambikiwa hizo gharama. Inabidi gharama za capacity charge zikokotolewe upya. Sasa ofisi ya CAG haina mamlaka ya kufanya ukokotoaji huo.
“Kwa hiyo, kama ukokotoaji ungefanyika, labda tuseme IPTL ingetakiwa kutoza shilingi 20 kwa siku, maana yake ile tofauti ya shilingi 30 inayotozwa na shilingi 20 inayotakiwa kutozwa, yaani shilingi 10, ingekuwa ya Tanesco.
“Hii maana yake ni kwamba, katika kila shilingi 30 iliyokuwepo katika Escrow, ukiondoa zile za kodi, shilingi 20 zilikuwa za IPTL kwa sababu ya umeme wake iliyouza na shilingi kumi zilikuwa za Tanesco ambayo ni taasisi ya umma,” alisema.

HATUA ZA KINIDHAMU SAKATA LA ESCROW: BALOZI SEFUE APUMZISHA MASWI KAZI.

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Ndg. Eliakimu Maswi

Dar es Salaam. Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue amemsimamisha kazi kwa muda, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakimu Maswi ili kupisha uchunguzi wa tuhuma kuhusu ushiriki wake katika sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow.

Badala yake, Sefue amemteua Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Ngosi Mwihava kukaimu nafasi ya Maswi hadi uchunguzi husika utakapokamilika.

Maswi (pichani), anakuwa kiongozi wa tatu kukumbwa na dhoruba inayotokana na sakata la Escrow baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Mwanasheria Mkuu, Jaji Frederick Werema na kung’olewa kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka juzi.
Hatua ya Balozi Sefue inafanana na ile iliyowahi kuchukuliwa na mtangulizi wake, Philemon Luhanjo Julai 21, 2011 pale alipomsimamisha kazi kwa muda aliyekuwa Katibu Mkuu katika wizara hiyo, David Jairo na kukaimisha nafasi yake kwa Maswi ili kupisha uchunguzi.
Baadaye Jairo alirejeshwa kazini lakini siku moja baadaye Rais Kikwete alimrejesha nyumbani kutokana na shinikizo la wabunge na tangu hapo hakuwahi kurudi katika utumishi wa umma na badala yake Maswi alithibitishwa kuwa katibu mkuu hadi jana.
Hatua ya kusimamishwa kwa Maswi imekuja siku moja tangu Rais Jakaya Kikwete alipoelekeza mamlaka za utumishi kuchukua hatua dhidi ya Maswi baada ya kufanya uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazomkabili.
“Kuhusu katibu mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, kwa vile ni mtumishi wa umma, anatawaliwa na sheria na kanuni za utumishi wa umma, hivyo nimeshaelekeza mamlaka kuchunguza tuhuma zake na hatimaye ikibainika ana makosa hatua za kinidhamu zitachukuliwa,” alisema Rais Kikwete wakati akilihutubia Taifa kupitia wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam juzi.
Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu jana, ilisema Balozi Sefue amechukua hatua hiyo kwa kutumia madaraka aliyonayo kama mamlaka ya nidhamu kwa watumishi wa umma wanaoteuliwa na Rais, wakiwamo makatibu wakuu.
Amechukua hatua hiyo kwa mujibu wa Kifungu 4(3) (d) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Namba 8 ya 2002 (kama ilivyorekebishwa). Maswi na watumishi wengine wa umma ambao wametajwa watashughulikiwa na Tume ya Maadili, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa (Takukuru) pamoja na Jeshi la Polisi na ikithibitika kuwa walikiuka maadili yao ya kazi, sheria stahiki zitachukuliwa.

JK: FEDHA ZA TEGETA ESCROW NI ZA IPTL



Rais Jakaya Kikwete akihutubira wazee wa mkoa wa Dar es Salaam
kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini hapa.
Dar es Salaam. Rais Jakaya Kikwete amesema fedha zilizochotwa katika Akaunti ya Tegeta Escrow hazikuwa zinafikia Sh306 bilioni, bali ni Sh202 bilioni na zilikuwa mali ya Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL.

Akijibu swali alilojiuliza mwenyewe katika hotuba yake ya zaidi ya saa mbili kuwa: “Fedha hizi mwenyewe nani, umma au IPTL?” Rais Kikwete alisema kumekuwapo na maneno mengi, kila mtu anasema yake na wenzangu Wakwere tunasema ‘tunazoza sana’ akimaanisha waongea sana.

Alisema, “Kimsingi fedha hizi ni za IPTL, katika swali pesa za nani, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) alipoulizwa na Kamati ya Bunge alisema humu yawezekana zipo za umma pia zipo za IPTL.

“Nilipomuuliza maana, akasema zamani walikuwa wanalipa moja kwa moja kwa Tanesco lakini baada ya mzozo walikubaliana kwanza waziweke Benki Kuu ya Tanzania (BoT).”

Akielezea maana ya escrow, alisema, “Ni tofauti kidogo na akaunti zetu tatu tulizozizoea, ni akaunti maalumu ya kazi maalumu na kazi hiyo maalumu ikiisha inafungwa. Inasimamia na wakala na wakala pia ana jukumu la kumlipa mwenye fedha wakati ukifika.”

Ukumbi uliojaa wazee na wasio wazee wakimsikiliza kwa umakini ulikuwa umetulia kimya alipoanza kuzungumzia sakata hilo, akisema akaunti hiyo ilifunguliwa BoT kwa ajili ya kuweka fedha za tozo ya uwekezaji, ili kutoa nafasi kwa pande mbili kushughulikia tofauti zao.

“Kama mgogoro ungetatuliwa na madai ya Tanesco yakakubaliwa na tozo kupunguzwa, katika kiasi kilichopunguzwa kuna pesa za Tanesco ambazo lazima zirudi, bahati mbaya miaka saba baadaye hilo (la maelewano) halikuwa limefanyika.”

“Kama katika fedha hizo ipo kodi ya Serikali na kwa mujibu CAG kulikuwa na Kodi ya Ongezeko la Thamani (Vat) ambayo haikulipwa, IPTL hawakuilipa na uthamini ulikuwa zaidi ya Sh21.7 bilioni na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imepeleka madai yake kwa PAP,” alisema Rais Kikwete.

Aliongeza: “CAG aliwaelekeza Tanesco kuacha kuhesabu fedha walizolipa kwenye Akaunti ya Escrow kama yao, pesa hazikufikia sifa kuhesabika kama mali ya Tanesco. Mahakama Kuu ya Tanzania ilifanya uamuzi katika shauri la maombi ya VIP, kusimamisha mchakato wa ufilisi wa IPTL na Mahakama ikakubali.”

Alisema Wizara ya Nishati na Madini ilimwandikia Mwanasheria Mkuu wa Serikali (wakati huo), Jaji Frederick Werema kuomba ushauri na aliwashauri; “walipeni, uamuzi uko sawa na hauna matatizo na BoT waliuliza maswali hayohayo na majibu yakawa yaleyale.”

Alisema: “Kwa kuzingatia ushauri huo akaunti ikafungwa na pesa kukabidhiwa PAP. Mjadala ukaendelea bungeni na kwenye mablogu. Hata Tanesco ilipewa ushauri huohuo, uamuzi ule umetiliwa shaka na kuonekana haukuwa sahihi na umeitia hasara nchi. Ukaibua hisia na ni kwa sababu nzuri tu kwamba si bure na iko namna kama ya rushwa na watu kunufaika binafsi. Mara kuna watu wamekwenda benki na kubeba pesa viroba, kwenye sandarusi, lumbesa na mengineyo.”

Alisema, “Nilipokutana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, alisema hakukosea katika ushauri wake na wala Mahakama haikufanya makosa na huo ndiyo ulikuwa msimamo wake na mpaka sasa bado anaamini hivyo kuwa fedha si mali ya umma.

“Kuhusu hasara iliyopatikana alisema hakuna hasara yoyote iliyopatikana kwa sababu fedha ililipwa kwa mtu halali. Kwa upande wa kodi ya Serikali ambazo hazikulipwa, AG alipoulizwa alisema hakuna kodi iliyochelewa kulipwa. Yamesemwa mengi na bado hatujamaliza kuyasoma, rushwa ni kosa la jinai. Nilielekeza taarifa walizozipata wazipeleke Takukuru. Nimeambiwa wanaendelea na mchakato wao.