Rais
wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr.Ali Mohamed Shein
amemuapisha mwanasheria mkuu mpya wa Zanzibar Said Hassan Said akichukua nafasi
ya Bw. Othman Masoud.
Hafla
ya kumuapisha Bw. Said ilifanyika ikulu ya Zanzibar Jana (Friday , 17th Oct ,
2014) na
kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa seriklai akiwemo makamu wa kwanza wa Rais
Malim Seif Sharrif Hamad, Waziri wa Bishara Viwanda na Masoko Mhe. Nassor
Mazrui, mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibu Abdullah Mwinyi, Mufti mkuu wa Zanzibar
Sheikh Saleh Omar Kabi, Mstahiki Meya wa Zanzibar Mhe. Abdulrahman Khatibu na
vingozi wengine wa serikali.
Uteuzi
wa Bw Said Hasan Said ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa naibu mwanasheria mkuu
imekuja baada ya Dr Ali Shein Rais wa Zanzibar kumfuta kazi mwanasheria mkuu wa
Zanzibar Bw Othman Masoud Othman wiki iliyopita huku kukiwa hakuna sababau
yeyote iliyotolewa na serikali.
Ingawa
Duru za siasa zianoyesha wazi wazi kuwa kufutwa kwake kazi ni kutokana na
kupinga baadhi ya vifungu vya Katiba Inayopendekezwa wakati wa upigaji kura na
kabla ya hapo kujiondoa katika kamati ya uandishi wa Katiba hiyo.
No comments:
Post a Comment