Rais
Obama amesema wanajeshi hao wataongeza nguvu ya jeshi katika kutoa misaada ya
kibinadamu katika eneo hilo. Kundi
la kwanza la wanajeshi hao linatarajiwa kupelekwa kusaidia ujenzi wa vituo 17
vya kutolea tiba ya ugonjwa huo, katikati mwa Liberia, moja ya nchi
iliyoathiriwa vibaya na ugonjwa huo.
Maafisa
wa kikosi cha ulinzi wameelezea agizo hilo la Raisi Obama kama agizo la muhumu
ili kuongeza kasi ya kutekeleza mipango ya kwenda kuisaidia mapambano ya
ugonjwa huo na
itamfanya rais kutuma majeshi mengine zaidi iwapo watahitajika. Marekani
imeahidi kupeleka askari wake wapatao elfu nne huko Africa Magharibi kusaidia
mapambano ya kuzuia na kuumaliza kabisa ueneaji wa ugonjwa wa Ebola.
Rais
Obama amesema hajapinga wazo la kutekeleza katazo la kuziuia watu wanaoingia
nchini Marekani kutoka nchi zilizo athiriwa na ugonjwa huo,na hadhani kama wazo
hilo litafanikiwa. Ameyasema
hayo mwishoni mwa mkutano aloufanya katika ikulu ya Marekani na maafisa wa
shirikisho juu ya ushiriki wa nchi ya Marekani katika mapambano na ugonjwa huo.
Raisi Obama amesema anaamini hatua za uchunguzi wa ugonjwa huo ni hatua nzuri. Sina sababu za kifolosofia ya kupinga katazo la safari, kama hiyo ndiyo itakuwa ndiyo njia bora ya kuwaweka raia wa Marekani salama.tatizo ni kwamba je haya ndiyo majadiliano yangu niliyoyafanya a na wataalamu walioko kwenye maeneo ya tukio yaliyoathiriwa na ugonjwa huo ni kwamba katazo la safari halina nguvu kama hatua tulizochukua hivi karibuni kupambana na ugojwa huo.
Obama
pia aesema yupo wazi kumteua atakayesimamia janga la Ebola. Mpaka
hatua hii kila mtu binafsi amefanya kazi nzuri yenye kutukuka ,kazi ambayo ni
ngumu kupambana na majimaji ya ugonjwa huu. Hii inatufanya tuwe kama mtu mmoja
,kwa sehemu baada ya janga hili tunaweza kusonga mbele kama kawaida.
Naye
mkuu wa kitengo cha maendeleo ya kimataifa wa Marekani ameahidi kuongeza dola
milioni mia moja na arobaini na mbili ili kusaidia mapambano ya ugonjwa wa
Ebola huko Guinea. Bwana
Rajiv Shah aliyeko nchini Guinea kwenye ziara ya kujionea hali halisi ya athari
zilizoletwa na ugonjwa huo Africa Magharibi, na kusema kwamba anafikiri msaada
huo utarejesha matumaini ya watu waishio nchini humo.
Natangaza
ongezeko la dola milioni moja na eflfu arobaini na mbili ili kuendeleza
mapambano nchini Guinea katika ugonjwa wa Ebola,kwa vitengo vinavyojihusisha na
ugonjwa huu,ili kuongeza ufanisi katika idara ya afya na wafanyakazi wake na
kuongeza nguvu katika elimu juu ya ugonjwa huu.
No comments:
Post a Comment