To Chat with me click here

Thursday, June 27, 2013

UCHAGUZI MKOANI ARUSHA WAAHIRISHWA BAADA YA MLIPUKO WA BOMU



Mwk. wa NEC, Damian Lubuva

Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania (NEC) imeusogeza mbele uchaguzi kwenye wadi nne za Arusha kutoka tarehe 30 Juni hadi 14 Julai ili hali itulie, liliripoti gazeti la Daily News la Tanzania siku ya Jumatano (tarehe 26 Juni).

Uchaguzi huo uliahirishwa kutokana na ghasia zinazoendelea baada ya mlipuko wa bomu kwenye mkutano wa kampeni wa chama cha upinzani cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mapema mwezi huu.

"Kwa bahati mbaya tumegundua kwamba hali bado haijakuwa sawa na inahitaji muda zaidi kuchunguzwa," alisema Mwenyekiti wa NEC, Damian Lubuva. "Tunataka watu wapige kura kwa amani ... Wapiga kura wanaweza kufanya maamuzi yasiyo busara au yatokanayo na taarifa mbaya ikiwa watapiga kura katika hali ya wasiwasi."

Lubuva aliwakumbusha wagombea na vyama kwamba uahirishaji huo haukukusudiwa kuruhusu kampeni zaidi kuendelea.

KENYA YATISHIA KUCHUKUA HATUA KALI DHIDI YA VURUGU ZA KOO


Maofisa wa usalama wa Kenya Jumatatu wakionyesha silaha zilizokamatwa wakati wa mapigano ya koo katika wilaya ya Rhamu, Kaunti ya Mandera.

Polisi huko kaskazini mashariki mwa Kenya wameimarisha usalama katika kaunti ya Wajir kuzuia vurugu zilizoenea kutoka Kaunti jirani ya Mandera baina ya koo za Degodia na Gare.


Vurugu za hivi karibuni ziliibuka huko Wajir zilianza Ijumaa iliyopita (tarehe 21 Juni) wakati wanaume washukiwa wa koo za Degodia walipovamia malori mawili katika kijiji cha Eldas, na kuua wanaume wanne wa koo za Gare, Mkuu wa Kaunti ya Wajir Naftali Mung'athia alisema.

Katika kulipiza kisasi kwa mfululizo wa mashambulio ya hivi karibuni dhidi ya Gare, wanaume wenye silaha walivamia kambi ya watu wasio na makazi ndani ya nchi katika wilaya ya Banisa ya Kaunti ya Mandera, na kuua watu 14 ikiwa ni pamoja na ofisa polisi Jumapili. Waliokufa, ni pamoja na wanawake na watoto, wote kutoka ukoo wa Degodia.
Baadhi ya Familia zilizokosa makazi.

Jumatatu, kundi la watu kutoka katika ukoo wa Degodia waliwalenga watu kutoka ukoo wa Gare katika ghasia kwenye mji wa Wajir, walimuua mwanamke mmoja na mwingine kujeruhiwa vibaya baada ya kukanyagwa na msafara uiokuwa ukibeba familia zilizokuwa zikikimbia vurugu hizo.

Kuepusha mapigano zaidi baina ya koo mbili hizo, mamlaka zinazohusika zimesambaza maofisa usalama na askari katika viunga vyote vya jirani na Wajir, Mung'athia alisema. Alitoa wito kwa wakaazi wa Wajir kuwa watulivu wakati serikali ya Kaunti ikifanya kazi kutatua mzozo huu, akiongezea kwamba upigaji marufuku wa muda wa mikusanyiko imetekelezwa. 

"Tunafanya kazi mchana na usiku kuzuia mzozo kutokuendelea," Mung'athia alisema. "Tumewataka viongozi wa ndani na maulamaa kuungana katika kurejesha amani baina ya koo hizi."

Historia yenye vurugu

Wimbi la hivi karibuni la vurugu hizi lilianza mwezi Machi wakati wa gari la kampeni linalomilikiwa na mgombea seneta Billow Kerrow, ambaye anatoka katika ukoo wa Gare, lilipomgonga na kumuua mfanyabiashara kutoka katika ukoo wa Degodia huko Rhamu. Baadhi ya wanachama wa jumuiya ya Degodia walidai ajali ilikuwa imepangwa.

Kutoka hapo, mapigano ya koo, na mashambulizi ya kulipiza kisasi yameshaua watu zaidi ya 50 na kufanya mamia ya familia kukosa makazi. 

Vurugu baina ya koo mbili hizio yamekuwa yakipamba moto siku hadi siku, na yalianza kuongezeka kutoka mwaka 1984 wakati ukame uliposababisha mzozo wa maeneo ya malisho, kwa mujibu wa Mkuu wa Kaunti ya Mandera Michael ole Tialal.

Gare ni ukoo unaotawala huko Mandera, wakati Degodia ni wengi huko Wajir.
Usambazaji mdogo wa maji na ardhi ya malisho yamekuwa ni maeneo ya mzozano kati ya koo hizo, Tialal alisema, akiongeza kwamba kuenea kwa bunduki katika mpaka wa Somalia na Ethiopia kumeongeza vurugu katika tatizo la usalama la mkoa. 

"Ni mara ya kwanza kwa ukoo kutumia chombo cha kurushia maguruneti katika mapigano yao ya koo," Tialal alisema, akirejea shambulio kwenye kambi katika wilaya ya Banisa. "Vurugu hizo pia zilihusisha kuchoma nyumba na kuvamia magari." 

"Kwa sasa tunatoa kikundi cha walinzi cha wasindikizaji wenye silaha na magari yanashauriwa kusafiri kwa kusindikizwa na ulinzi ili kupunguza [uwezekano wa] shambulio,".

Siku ya Jumatatu, Inspekta Jenerali wa Polisi wa Kenya David Kimaiyo aliwaita viongozi waliochaguliwa wa kaunti za Mandera na Wajir katika idara ya Uchunguzi wa Makosa ya Jinai kuhusiana na ripoti za upelelezi zikionyesha kwamba mashambulizi "yalichochewa kisiasa".

Baada ya kukutana Nairobi siku ya Jumatatu na viongozi wa kaunti zote mbili, Rais Uhuru Kenyatta alisema serikali ya Kenya inaweza kutumia nguvu kurejesha amani katika mkoa wa kaskazini-mashariki, akiagiza jamii zinazopigana kusalimisha silaha haramu. 

"Kama jamii za kaunti za Mandera na Wajir hawatarejesha amani wao wenyewe, serikali itakuwa haina lingine la kufanya bali kutumia operesheni ya ulinzi ambayo inaweza kutokuwa na matokeo yasiyodhamiriwa," rais alisema.
Pia Kenyatta aliahidi kufanya kazi na serikali ya Ethiopia kuhakikisha kuishi pamoja kwa amani miongoni mwa jamii nyingine za kikabila zilizoenea katika mkoa ambako mipaka ya Kenya, Ethiopia na Somalia inakutana.

OBAMA EMBARKS ON THREE-COUNTRY AFRICA TRIP



The president touches down in Africa for a week-long visit as the continent monitors the declining health of Nelson Mandela.

The First Family arrives at the airport in Dakar, Senegal
President Barack Obama has kicked off the first leg of a three-country visit to Africa - his most extensive trip to the continent as president. Air Force One touched down in the Senegalese capital of Dakar on Wednesday night.
 
The president was accompanied by First Lady Michelle Obama and daughters Malia and Sasha.

Mr Obama's trip is highly anticipated given his personal ties to the continent. His father was born in Kenya and many of his relatives still live there. However, the president has spent just one day in Africa since taking office - a 2009 day trip to Ghana. In addition to Senegal, he will visit South Africa and Tanzania during this week-long trip.

Looming over Mr. Obama's visit is the deteriorating health of former South African President Nelson Mandela.

Michelle Obama and her daughters met Mr Mandela during a trip in 2011
Few major policy announcements are expected during Mr. Obama's trip. Instead, the president will focus on promoting democratic institutions, boosting opportunities for Africa's vast youth population and promoting the continent as a growing market for US businesses.
 
The White House defended the purpose of the trip despite its low policy expectations.

"Presidential trips to regions of the world like Africa bring enormous benefits in terms of our relationship with the countries visited and the countries in the region," spokesman Jay Carney told reporters travelling on Air Force One.
"The trip itself will not be the end point of our engagement, but will enhance it, deepen it and further it," he said.

The president will make two stops at sights that highlight the continent's harsh racial history: Senegal's Goree Island, which was the centre of Atlantic slave trade.

He also will visit Robben Island, the apartheid-era prison in South Africa where Mr Mandela spent 18 years of his 27 years in prison.

MANDELA: SOUTH AFRICAN PRESIDENT CANCELS TRIP



Former SA President Nelson Mandela with member of his family.

President Jacob Zuma has cancelled a trip to Mozambique, as the goverment says Nelson Mandela's condition "remains critical". Mr Zuma decided to stay in South Africa after visiting Mr Mandela in hospital where he "found him to be still in a critical condition", according to a statement from the President's office.
 
The announcement comes after sources confirmed to Sky News that Mr Mandela was no longer able to breathe unassisted.

The 94-year-old anti-apartheid leader was taken to a Pretoria hospital with a recurring lung infection on June 8, where he has now been treated for 19 days. The cancellation of the trip to Mozambique, which was scheduled for today, is the first time Mr Zuma has scrapped a public engagement during that time.
 
"Nelson Mandela's tribal leaders have been told to prepare for the death of the former president, who remains in hospital unable to breathe without support".

"The advice comes after meetings with the family over the past two days. "Senior tribal leaders - including Mr Mandela's tribal heir, grandson Mandla Mandela - were expected to visit the hospital for further talks with family members.
 
People bring get well messages to Mr Mandela
"In the Eastern Cape, where Mr Mandela will be buried, a member of the tribal authority confirmed that the clan had been told that he is extremely ill and although it is against Xhosa tradition to even discuss the death of a living person, they should prepare for the worst."

The statement from the president's office said that Mr Zuma was briefed on Mr Mandela's condition by the doctors treating him. Speaking earlier in the week Mr Zuma said: "We must support him and support his family.
 
"We must demonstrate our love and appreciation for his leadership during the struggle for liberation and in our first few years of freedom and democracy by living out his legacy and promoting unity, non-racialism, non-sexism and prosperity in our country."

Thursday, June 13, 2013

KIDATO CHA SITA 2013 WANATAKIWA KURIPOTI JKT 24/06/2013



                                                         TANGAZO

Mkuu wa JKT Meja Jenerali Raphael Muhuga

MKUU WA JKT MEJA JENERALI RAPHAEL MUHUGA ANAWAITA VIJANA 10,849 WALIOHITIMU KIDATO CHA SITA MWAKA 2013 KUJIUNGA NA JKT KWA MUJIBU WA SHERIA KAMA IFUATAVYO:-

1. VIJANA WOTE WALIOHITIMU KIDATO CHA SITA WALIOPATA DIVISION I NA DIVISION II.

2. VIJANA WOTE WALIOHITIMU KIDATO CHA SITA WALIOSOMA MASOMO YA MCHEPUO WA SAYANSI NA KUPATA DIVISION III.

3. VIJANA HAO WANATAKIWA KURIPOTI KATIKA MAKAMBI YA JKT TAREHE 24 JUNI 2013 BILA KUKOSA. AMBAYE HATARIPOTI ATACHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA.

4. TANGAZO HILI HALIWAHUSU VIJANA WOTE WALIOHITIMU KIDATO CHA SITA 2013 KATIKA SHULE ZA SEKONDARI ZA UNGUJA NA PEMBA. AIDHA, SHULE 27 AMBAZO VIJANA WAKE WAMEHITIMU MAFUNZO YA JKT AWAMU YA KWANZA HAZIHUSIKI.

5. VIJANA HAO WATUNZE TIKETI ZAO KWA AJILI YA KUREJESHEWA NAULI WATAKAZOTUMIA MARA TU WATAKAPORIPOTI VIKOSINI.

6. TAARIFA ZAIDI ZITATOLEWA KWENYE MAGAZETI MBALIMBALI YA HAPA NCHINI.

============================== =====

Selections hizi hapa:
Endepo tovuti ya JKT itakuwa ngumu kufunguka, angalia hizi attachments from JF