Mvua kubwa iliyonyesha jana kwa karibu siku nzima, zilileta maafa makubwa kwa wakazi wa jiji la Dar-es-Salaam, ambapo kumeripotiwa kuwa baadhi ya nyumba hasa maeneo ya mabondeni ziliangushwa na mvua hizo. Pia vyanzo vyetu vya habari vinazidi kueleza kuwa, baadhi ya sehemu za jijini, barabara zilikuwa zimefunikwa na maji kabisa kutokana na miundo mbinu kutokuwa sawa katika baadhi ya maeneo katika jiji hili. Mbali na hayo pametokea shida kubwa ya usafiri kwa wakazi wa jiji kwani, mkagari mengi yalionekana kupaki na machache mno kutoa huduma ya usafiri kwa wakazi wa jiji hivyo kusababisha mikusanyiko mikubwa ya watu vituoni.
Moja kati ya barabara za jijini maeneo ya Yombo Vituka ikiwa imefunikwa na maji kabisa, kutokana na mvua kubwa zilizo nyesha jana, hivyo kusababisha usafiri kuwa mgumu sana hususani maeneo hayo.
Baadhi ya magari ya abiria yakiwa yamepaki na machache kuonekana yakitoa huduma ya usafiri kwa abiria ambao walionekana kuwa ni wengi kuliko magari kwa siku ya jana.
Kutokana na mvua za jana kunyesha kwa mfululizo, ziliweza kuleta maafa kwa baadhi ya wakazi wa Dar-es-Salaam, vilevile kuharibu baadhi ya miundombinu pia kubomoa baadhi ya nyumba katika jiji hili maarufu. Kama tunavyojionea hapo pichani.
No comments:
Post a Comment