Mbunge Mteule wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Mhe. Joshua Nassari akitoa kiapo cha utiifu na uaminifu Bungeni mjini Dodoma baadaya ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo katika uchaguzi uliofanyika Jumapili ya tarehe 1 aprili mwaka huu huko Arumeru. Mhe. Nassari amekuwa mbunge wa Jimbo hilo kwa tiketi ya CHADEMA baada ya kumshinda mpinzani wake wa karibu toka chama cha CCM ndugu Sioi Sumari, ambaye pia baba yake mzazi ndiye aliyekuwa akishikiria kiti cha ubunge wa jimbo hilo kabla ya kukutwa na umauti miezi michache iliyopita.
Hii ni Hati ya Ushindi aliyokabidhiwa Mhe. Joshua Nassari na Tume ya Uchaguzi/Msimamizi wa Uchaguzi huo mdogo, hivyo na kumtangaza rasmi kuwa yeye ni mshindi wa Kiti hicho, siku moja baada ya kura kuhesabiwa. Tunapenda kumpa pongezi Mhe. Nassari na tunamtakia uwajibikaji wa dhati kwa wananchi wa Arumeru Mashariki.
No comments:
Post a Comment