To Chat with me click here

Wednesday, April 24, 2013

UGUMU WA UPATIKANAJI WA AJIRA KWA VIJANA CHANZO CHA MAOVU

Baadhi ya Vijana ambao wamekuwa wakishinda mitaani na kuzunguka huku na huko kujitafutia riziki zao za kila siku, wamejikuta wakiingia katika makundo tofauti tofauti ya uovu pasipo wao wenyewe kujijua kuwa wamekwisha anza kuharibikiwa. 

Baadhi ya vijana waliohojiwa na mwana-habari wetu wa blog hii, wametupia lawama nyingi serikali ya awamu ya nne, wakisisitiza kuwa; serikali ndiyo inasababisha maisha kuwa magumu na kutokuwa na upatikanaji wa ajira kwa vijana.

"Serikali kwa kweli kabisa haina nia ya dhati ya kututoa katika tatizo hili la ajira, kwani mimi binafsi sioni inafanya nini kupunguza tatizo" alisema kijana mmoja. 

Kijana mwingine alisema; "Yani, hawa jamaa wako kwa ajili ya kushibisha matumbo yao tuu, kwani maisha kila siku yanakuwa magumu, na hiyo inatokana na wao kushikiria uchumi mikononi mwao, hivyo wanatuendesha watanzania jinsi wanavyotaka". 

Mwandishi wetu alifanya mahojiano na vijana hao ambao walikuwa wakikusanya nondo toka kwenye mabaki ya baadhi ya vifusi vya nyumba vilivyobomolewa maeneo ya Yombo Vituka, Temeke. Inasemekana kwamba baadhi ya vijana asubuhi ya leo walikamatwa na kufikishwa kituo cha polisi chang'ombe baada ya kukamata wakiwa wameiba sehemu ya nondo hizo na kuziuza kwa wanunua vyuma chakavu.

 
Vijana wakishughulika katika maeneo hayo.

No comments:

Post a Comment