To Chat with me click here

Monday, April 29, 2013

CHADEMA YAISAMBARATISHA CCM UCHAGUZI WA VIJIJI KILOSA




Chama cha CHADEMA kimezidi kuonyesha umwamba dhidi ya CCM katika uchaguzi wa kijiji na kitongoji huko Kilosa.
 
Taarifa zilizoingia hivi punde zinasema katika uchaguzi wa Mkiti kijiji cha Kifinga CHADEMA imeshinda kwa kura 450 dhidi ya 150 za CCM.
 
Katika uchaguzi wa Mkiti wa Kitongoji cha Ruaha B CHADEMA imeibuka na ushindi wa kura 600 dhidi ya kura 250.

Wednesday, April 24, 2013

UGUMU WA UPATIKANAJI WA AJIRA KWA VIJANA CHANZO CHA MAOVU

Baadhi ya Vijana ambao wamekuwa wakishinda mitaani na kuzunguka huku na huko kujitafutia riziki zao za kila siku, wamejikuta wakiingia katika makundo tofauti tofauti ya uovu pasipo wao wenyewe kujijua kuwa wamekwisha anza kuharibikiwa. 

Baadhi ya vijana waliohojiwa na mwana-habari wetu wa blog hii, wametupia lawama nyingi serikali ya awamu ya nne, wakisisitiza kuwa; serikali ndiyo inasababisha maisha kuwa magumu na kutokuwa na upatikanaji wa ajira kwa vijana.

"Serikali kwa kweli kabisa haina nia ya dhati ya kututoa katika tatizo hili la ajira, kwani mimi binafsi sioni inafanya nini kupunguza tatizo" alisema kijana mmoja. 

Kijana mwingine alisema; "Yani, hawa jamaa wako kwa ajili ya kushibisha matumbo yao tuu, kwani maisha kila siku yanakuwa magumu, na hiyo inatokana na wao kushikiria uchumi mikononi mwao, hivyo wanatuendesha watanzania jinsi wanavyotaka". 

Mwandishi wetu alifanya mahojiano na vijana hao ambao walikuwa wakikusanya nondo toka kwenye mabaki ya baadhi ya vifusi vya nyumba vilivyobomolewa maeneo ya Yombo Vituka, Temeke. Inasemekana kwamba baadhi ya vijana asubuhi ya leo walikamatwa na kufikishwa kituo cha polisi chang'ombe baada ya kukamata wakiwa wameiba sehemu ya nondo hizo na kuziuza kwa wanunua vyuma chakavu.

 
Vijana wakishughulika katika maeneo hayo.

ZANZIBAR YETU LEO !


Hii ndiyo Zanzibar ilivyokuwa leo...............

 Jengo la Baraza la Manispaa Zanzibar kama lionekanavyo pichani.
 Jumba la Makumbusho - Zanzibar
 Hii ni Wizara ya Utamaduni, Michezo na Utalii - Zanzibar
 

 Mambo ya TENDE ndani ya Zenj hapo.

Saturday, April 13, 2013

LWAKATARE ALIGAWA BUNGE



SAKATA la Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare na Ludovick Rwezaula kushtakiwa kwa makosa ya ugaidi, limeibua mvutano mkali bungeni huku wabunge wakishambuliana kwa maneno makali.

Mvutano huo uliibuka jana wakati wa kujadili hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2013/2014 ambapo Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba (CCM) alichafua hewa wakati akichangia na kudai kuwa aliyerekodi video ya Lwakatare yupo tayari kuja kutoa ushahidi.
Mwigulu ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) aliliambia Bunge kuwa CHADEMA wasihangaike kujitetea kwa swala la Lwakatare kwani ushahidi wote kuhusu video hiyo upo na kwamba yuko tayari kuutoa bungeni, duniani na mbinguni.

“Nataka nitoe ufafanuzi kuhusu suala la ugaidi ambalo Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amezungumza kwenye hotuba yake hapa bungeni jana. Aliyerekodi mkanda yupo na mimi niko tayari kuhojiwa popote hata mbinguni,” alisema Mwigulu na kuibua nderemo kutoka kwa wabunge wa CCM.

Mwigulu alionyesha karatasi aliyodai kuwa ilitumiwa na Lwakatare kupanga kile alichodai kuwa ni mkakati wa mauaji akisema huo ndiyo mkakati wa CHADEMA kupanga mauaji na kwamba viongozi wakuu wa chama hicho wanapaswa kushtakiwa.

Bila kujali kwamba suala hilo liko mahakamani wala ni kinyume cha kanuni za Bunge kumtaja mbunge mwingine kwa jina akimtuhumu, Mwigulu alisema anaishangaa CHADEMA kumtaka yeye aunganishwe kwenye kesi kwa kuwa na mawasiliano na mmoja wa watuhumiwa wakati hata wao wana mawasiliano na Lwakatare.

“Alisema Mbowe hapa jana kuwa mimi napaswa kushtakiwa kwa ugaidi, ingawa simuoni hapa ndani labda tayari amekwishakamatwa na polisi, lakini nataka kusema kuwa watu hawa ni waongo na wanafiki. Wanapanga mauaji halafu wanakuja hapa kuwahadaa wananchi kuwa wanapinga ugaidi,” alidai.

Hatua hiyo ya Mwigulu kumtaja Mbowe kwa jina na chama chake kuwa ni magaidi, iliwashtua baadhi ya wabunge wakishangaa kuona Spika wa Bunge, Anne Makinda akishindwa kutumia kanuni kumbana na kumtaka afute kauli ana atoe uthibitisho.

Baada ya kuona Makinda anakuwa na kigugumizi, baadhi ya wabunge wa CHADEMA, Joseph Selasini (Rombo), Mustafa Akunaay (Mbulu), Pauline Gekul (Viti Maalumu) walijaribu kusimama kuomba mwongozo lakini walikataliwa.

Thursday, April 11, 2013

KADA CHADEMA AZIDI KUTESWA


JESHI la Polisi Makao Makuu limeendelea kumshikilia kwa siku 11 bila kumfikisha mahakamani Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la CHADEMA (BAVICHA) mjini Bukoba, Evodius Justinian (30) huku ndugu zake wakizuiliwa kumpa chakula isipokuwa maji tu.

Justinian alishikiliwa mjini Bukoba Aprili 2, mwaka huu kisha kusafirishwa hadi jijini Mwanza na kuhojiwa, kisha Dar es Salaam huku akipewa mateso makali ya kulazimishwa akubali kuhusika kutengeneza video inayomhusisha na uchochezi Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA, Wilfred Lwakatare.

Awali ndugu zake na viongozi wa CHADEMA mjini Bukoba walielezwa na polisi kuwa Justinian anasafirisha kwenda wilayani Igunga, Tabora ambako alidaiwa kuwa alitenda makosa ya jinai, lakini alifichwa jijini Mwanza.

Wakizungumza na gazeti hili, mawakili wa mtuhumiwa huyo Nyaronyo Kicheere na Peter Kibatala walisema kuwa juzi jioni ndugu zake walimpelekea chakula, lakini walipofika waliambiwa kuwa haruhusiwi chakula isipokuwa maji tu.

“Asubuhi alipelekewa chai, lakini polisi walidai kuwa ndugu walichelewa na hivyo kuwazuia. Na walipopeleka chakula cha mchana waliambiwa hayupo kwani alikuwa amepelekwa hospitali bila kuitaja kwa jina,” alisema Kicheere.

Kicheere aliongeza kuwa baada ya ndugu kuwapa taarifa hiyo, yeye na wakili mwenzake Kibatala walilazimika kuondoka mahakamani Kisutu walipokuwa wakimsubiri mteja wao afikishwe. Mawakili hao walisema wanakusudua wakati wowote kupeleka maombi Mahakama Kuu kudai polisi wapeleke mwili wa mtuhumiwa mahakamani (habeas corpus).

Lakini pia mawakili hao walisema kuwa leo wataendelea kushinda mahakamani muda wote wa kazi kumsubiri mteja wao. Waliwataka Watanzania wakiwemo wanasheria na watetezi wa haki za binadamu kuendelea kupiga kelele dhidi ya Jeshi la Polisi linavyokiuka haki za binadamu.

Akizungumzia hatua ya mtuhumiwa huyo kutofikishwa mahakamani kama ilivyokuwa imeahidiwa, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso alisema wakiwa tayari watasema na kuomba watu wasiingilie kazi yao.

“Tutasema siku ya kumfikisha, hapa suala la msingi ni polisi tunafanya nini, ni kama wewe unavyoandika habari, hakuna wa kukuuliza,” alisema Senso.

Alipoelezwa juu sheria inavyotaka mtuhumiwa kufikishwa mahakamani ndani ya saa 24 baada ya kukamatwa, Senso alisema pasipo kufafanua kuwa sheria hiyo hiyo inaweza kutumika vinginevyo. Jumatatu wiki hii, mbele ya wakili wake Kicheere, mtuhumiwa huyo alieleza unyama aliofanyiwa na jeshi hilo wakati wote wa mahojiano mkoani Mwanza na jijini hapa.

Katika maelezo yake yaliyoshuhudiwa na Ofisa wa Polisi Makao Makuu, Advocate Nyombi, Justinian alisema kuwa baada ya kutolewa mjini Bukoba kwa siri bila ndugu zake kujua, alipelekwa jijini Mwanza na kuhojiwa bila kuruhusiwa kuonana na wakili wake. Alieleza kuwa wakati wote wa mahojiano hayo alikuwa akilazimishwa kukiri kurekodi video ya Lwakatare inayoonesha mikakati ya ugaidi.

Alisema alisafirishwa kwa siri kwa ndege hadi Dar es Salaam, akapelekwa chooni na kupigwa, kutishiwa na kuteswa kwa nyaya za umeme na kunyimwa fursa ya kupewa chakula.

“Nimepigwa na polisi nikiwa Mwanza, nikiwa chooni Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam wakati naletwa huku, polisi wakaniambia mimi ni mtu hatari sana, niseme nilifanya nini Igunga. “Nikiwa Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam niliomba kwenda chooni, waliingia pamoja na mimi wakanipiga sana, nimeshaandika maelezo kwa kulazimishwa, niliomba kuwa na wakili wakanikatalia,” alisema.

Aliongeza kuwa akiwa Dar es Salaam alihojiwa aseme ukweli kuhusu video ya Lwakatare. Akawajibu kuwa ilifanyiwa uhariri na Ludovick, lakini akapigwa makofi na askari wakaagiza nyaya za umeme za kutesea.

“Waliposema kuleta nyaya za umeme, kwa kuhofia mateso ya umeme nikasema hii video ni yangu,” alisema.

Tanzania Daima.