Inadaiwa kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zinapokea misaada mingi
zaidi ya kigeni duniani; tena wapo wanaodai kuwa tuko katika 'top 3'.
Swali ambalo ninalo hasa baada ya wajomba zetu kuahidi kutoa mabilioni
mengine ni kuwa wakati upande mmoja tunapoteza fedha kwenye ufisadi tena
nyingi sana inakuwaje wajomba zetu wanaendelea kumimina mabilioni? Hivi hayo mabilioni yao hayawaumi kuona yanaliwa na wachache tuu na kutotumika kwa malengo husika? au misaada hiyo imelegwa makusudi kwa ajili yao ikiwa na malengo ya "nipe nikupe", kama ndivyo je watawala wetu wanamalengo gani na vizazi vya watanzania vijavyo?
Hivi wakiamua kusitisha misaada hii nini kitatokea kwenye uchumi na utendaji wa serikali yetu? Watanzania inabidi kujiuliza maswali haya sana na mwisho wa siku tufanye maamumzi makini ili kujinasua kwenye kitanzi tulichopo kwa sasa, kama si hivyo tuwe tayari kufa masikini na kumilikisha rasilimali zetu za nchi kwenye mikono ya wachache ambao wataendelea kuvuna na kuchumia matumbo yao na vizazi vyao vijavyo huku Watanzania wengine tukibaki tukilialia tu pasipo na pa kukimbilia. Hebu angalia jinsi grafu hii ioneshavyo;
Watafiti wengi wa mambo, wamekuwa wakisema kuwa Watanzania wengi wamechoshwa na haya yanayoendelea nchini lakini wamekuwa ni waoga wa kufanya mabadiliko, wakihofia je nini kitatokea baada ya mabadiliko? Lakini wapenda maendeleo na wanaharakati wengi wamekuwa wakiwaasa Watanzania kutokuwa waoga wa kufaya mabadiliko kwani "udhubutu" unaweza kuwakomboa toka katika kitanzi cha umasikini walichovikwa na watawala wetu wa sasa.
Ushauri wangu;
Mabadiliko ni lazima, hofu ya madiliko ni sawa na kuendelea kuukumbatia umasikini, kwani siku zote watu husema kuwa
"The risk takers are the very successful ones". Hivyo Watanzania wasiwe na hofu ya mabadiliko bali wawe na uthubutu wa kufanya maamumzi, lakini kwa uangalifu na umakini mkubwa.
No comments:
Post a Comment