To Chat with me click here

Saturday, April 14, 2012

KUAPISHWA KWA TUME YA KUKUSANYA MAONI JUU YA KATIBA MPYA

RAIS Jakaya Kikwete ametangaza Tume ya Mabadiliko ya Katiba itakayosimamia ukusanyaji wa maoni ya wananchi kuhusu uundwaji wa Katiba mpya ya Tanzania.
Tume hiyo inayoundwa na watu 34 itaongozwa na Mwenyekiti wake Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba, Makamu Mwenyekiti Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhan, Katibu ni Assad Ahmed Rashid na Naibu Katibu Casmir Sumba Kyuki.

Kuundwa kwa tume hiyo ni utekelezaji wa ahadi ya Rais Kikwete aliyoitoa Desemba 31 mwaka 2010 kwenye hotuba yake ya kuuaga mwaka ambapo alisema atahakikisha hadi kufikia mwaka 2014, Tanzania itakuwa na Katiba Mpya itakayokidhi matakwa ya Watanzania

Katika mkutano wake na Wahariri wa vyombo vya habari Ikulu jijini Dar es Salaam Rais Kikwete ameeleza namna tume hiyo ilivyoundwa kwa kuzingatia pande mbili za Muungano.

Rais ameweka wazi majina ya wajumbe 15 wanaounda tume hiyo kutoka Zanzibar kuwa ni Dokta Salim Ahmed Salim, Fatma Said Ali, Omar Sheha Mussa, Raya Suleiman Hamad, Awadh Ali Said, Ussi Khamis Haji, Salma Maoulidi, Nassor Khamis Mohammed, Simai Mohamed Said, Muhammed Yussuf Mshamba, Kibibi Mwinyi Hassan, Suleiman Omar Ali, Salama Kombo Ahmed, Abubakar Mohammed ALI na Ally Abdullah Ally SALEH.

Kwa upande wa wajumbe kutoka Tanzania Bara, Rais amewateua Profesa Mwesiga Baregu, Riziki Shahari Mngwali, Dokta Edmund Adrian Sengodo Mvungi, Richard Shadrack Lyimo, John Nkolo, Alhaj Said El- Maamry, Jesca Sydney Mkuchu, Profesa Palamagamba Kabudi, Humphrey Polepole, Yahya Msulwa, Esther Mkwizu, Maria Malingumu Kashonda, Al-Shaymaa Kwegyir, Mwantumu Jasmine Malale na Joseph Butiku.

Utata wa Wajumbe wa Kamati:

Rais akimwapisha Mhe. Al-Shaymaa Kwegyir, mbunge wa viti maalumu kuwa mmoja kati ya wajumbe wa kamati hiyo. (Utata)
Rais akimwapisha mwakilishi toka baraza la uwakilishi - Zanzibar (Utata)
Hapa akimwapisha Prof. Mwesiga Baregu - Mjumbe wa Kamati Kuu ya CDM na Mkuu wa kampeni yake 2010

Hapa anamwaipsha Dr. Sengodo Mvungi ambaye ni Mjumbe wa kamati kuu ya NCCR Mageuzi

Je! kulingana na sheria, kuna uhalali wa watu hawa kuwa wajumbe wa kamati ya kukusanya maoni ya Katiba mpya ikiwa sheria inakataza kabisa na waziwazi kuwa wabunge na wawakilishi au viongozi wa kisiasa wasiwe wajumbe wa Tume?  Je, huu si mgongano wa Kimaslahi kwa hawa wajumbe wa Tume wenye Utata? Au uwepo wa wajumbe hawa una maslahi kwa namna moja au nyingine kwa mheshimiwa sana?
  



JOSHUA NASSARI AAPISHWA BUNGENI

Mbunge Mteule wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Mhe. Joshua Nassari akitoa kiapo cha utiifu na uaminifu Bungeni mjini Dodoma baadaya ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo katika uchaguzi uliofanyika Jumapili ya tarehe 1 aprili mwaka huu huko Arumeru.  Mhe. Nassari amekuwa mbunge wa Jimbo hilo kwa tiketi ya CHADEMA baada  ya kumshinda mpinzani wake wa karibu toka chama cha CCM ndugu Sioi Sumari, ambaye pia baba  yake mzazi ndiye aliyekuwa akishikiria kiti cha ubunge wa jimbo hilo kabla ya kukutwa na umauti miezi michache iliyopita.   
Hii ni Hati ya Ushindi aliyokabidhiwa Mhe. Joshua Nassari na Tume ya Uchaguzi/Msimamizi wa Uchaguzi huo mdogo, hivyo na kumtangaza rasmi kuwa yeye ni mshindi wa Kiti hicho, siku moja  baada ya kura kuhesabiwa. Tunapenda kumpa pongezi Mhe. Nassari na tunamtakia uwajibikaji wa dhati kwa wananchi wa Arumeru Mashariki.  

Thursday, April 12, 2012

JE HUU NDIO UTAWALA WA KUFUATA SHERIA NA UHURU WA HAKI SAWA KWA KILA MWANANCHI?


Mama mmoja katika mitaa ya Arusha Mjini akiwa amebebwa na askari wa jiji juu bila hata kujali, utu wake huku wakiacha baadhi ya sehemu za mwili wa mama huyo zikiwa nje na huku baadhi ya raia wakifuatilia taflani hiyo.



Moja kati ya hospitali za baadhi ya vijiji vya Tanzania zikitoa huduma ya matibabu kwa wakina mama katika hali duni kabisa kama ionekanavyo pichani. Je kwa kasi hii tutafika kweli?

MVUA ZILIZONYESHA JANA ZALETA MAAFA NA KUKWAMISHA SHUGHULI ZA KIMAENDELEO

Mvua kubwa iliyonyesha jana kwa karibu siku nzima, zilileta maafa makubwa kwa wakazi wa jiji la Dar-es-Salaam, ambapo kumeripotiwa kuwa baadhi ya nyumba hasa maeneo ya mabondeni ziliangushwa na mvua hizo. Pia vyanzo vyetu vya habari vinazidi kueleza kuwa, baadhi ya sehemu za jijini, barabara zilikuwa zimefunikwa na maji kabisa kutokana na miundo mbinu kutokuwa sawa katika baadhi ya maeneo katika jiji hili. Mbali na hayo pametokea shida kubwa ya usafiri kwa wakazi wa jiji kwani, mkagari mengi yalionekana kupaki na machache mno kutoa  huduma ya usafiri kwa wakazi wa jiji hivyo kusababisha mikusanyiko mikubwa ya watu vituoni.

Moja kati ya barabara za jijini maeneo ya Yombo Vituka ikiwa imefunikwa na maji kabisa, kutokana na mvua kubwa zilizo nyesha jana, hivyo kusababisha usafiri kuwa mgumu sana hususani maeneo hayo. 


Baadhi ya magari ya abiria yakiwa yamepaki na machache kuonekana yakitoa huduma ya usafiri kwa abiria ambao walionekana kuwa ni wengi kuliko magari kwa siku ya jana.

Kutokana na mvua za jana kunyesha kwa mfululizo, ziliweza kuleta maafa kwa baadhi ya wakazi wa Dar-es-Salaam, vilevile kuharibu baadhi ya miundombinu  pia kubomoa baadhi ya nyumba katika jiji hili maarufu. Kama tunavyojionea hapo pichani.



Wednesday, April 11, 2012

MADAKTARI WATOA TAARIFA JUU YA CHANZO CHA KIFO CHA KANUMBA

Msanii nyota wa filamu nchini, Steven Kanumba amefariki kutokana na tatizo la mtikisiko wa ubongo linalojulikana kitaalamu kama BRAIN CONCUSSION, taarifa za kitabibu zimeeleza.

Taarifa hizo za ndani, zimepatikana jana baada ya jopo la madaktari bingwa watano wa hospitali ya taifa Muhimbili kuufanyia uchunguzi mwili wa marehem, zimeeleza kuwa tatizo hilo linaweza kumfanya mtu apoteze maisha mara moja au baada ya siku kadhaa.Mmoja wa madaktari hao ambae aliomba jina lake lisitajwe gazetini alisema waligundua tatizo hilo baada ya kumfanyia uchunguzi huo kwa zaidi ya masaa mawili.

"tulianza kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 6:45 mchana na tukagundua kuwa marehemu alifariki kutokana na mtikisiko wa ubongo kwa kitaalamu Brain Concussion" alisema. Kanumba alipata mtikisko huo ambao husababisha kufeli kwa mfumo wa upumuaji (cardio-respiratory failure) "kilichomuua hasa ni mtikisiko wa ubongo, ambao endapo unatokea katika sehem ya nyuma ua ubongo (cerebram), huua kwa haraka" alisema daktari huyo na kuongeza kuwa mtikisiko wa ubongo wa nyuma husababusha matatizo ya mfumo wa upumuaji na hilo limeonekana katika mwili wake.

"Baada ya ubongo wake kutikiswa kwa nguvu, mfumo wa upumuaji unafeli na ndio maana tumekuta kucha za kanumba zikiwa na rangi ya blue, huku mapafu yake yakiwa yamevilia damu na kubadilika kuwa kama maini, hizo ni dalili za kufeli kwa mfumo wa upumuaji"

"Mtu aliepata mtikisko wa ubongo huweza kutokwa na mapovu mdomoni na hukoroma kabla ya kukata roho na ndivyo ilivyokuwa kwa Kanumba kabla hajafariki.

Daktari mwingine alieshiriki katika uchunguzi huo ambae pia aliomba jina lake lisitahwe alisema ubongo wa mwigizaji huyo umevimba na kushuka karibu na uti wa mgongo na hivyo kuathiri mfumo wa upumuaji. Alisema sehemu ya maini na maji maji ya machoni ya marehemu, vimepelekwa kwa mkemia mkuu wa Serikali ili kubaini endapo kuna sumu au kitu kingine katika mwili huo

Mungu ailaze roho ya marehemu Kanumba mahali pema peponi AMINI

MSIBA WA KANUMBA ....

Maelfu ya waombolezaji wakiwa wanausindikiza mwili wa marehemu Kanumba katika makazi yake ya milele katika makaburi ya Kinondoni Dar-es-Salaam.
Mwili wa marehemu Steven Kanumba ukiteremshwa kwenye nyumba yake ya milele mara baada ya taratibu zote za kumuuga kumamilishwa katika viwanja vya leaders club hapo jana.
Mwili wa aliyekuwa muugizaji wa Filamu Tanzania ndg. Steven Kanumba mara baada ya kuwasili katika makaburi ya Kinondoni Dar es Salaam, kwa ajiili ya mazishi yake hapo jana jioni majira ya saa kumi jioni.
Mwili wa Marehemu Steven Kanumba ukiondolewa katika viwanja vya Leaders Club ukielekea makaburi ya Kinondoni kwa ajili ya mazishi yake, huku kila aliyekuwepo akitaka hata kugusa gari lililokuwa limebeba mwili huo.
Kila mtu alikuwa akitaka hata alisogelee au hata kushika au kuiona tu picha ya marehemu kanumba, kwa kweli alikuwa akipendwa na watu. 
Mwili wa Marehemu Kanumba ukianza kuondolewa tayari kwa kuanza safari yake ya mwisho kuelekea katika makaburi ya kinondoni kwa ajili ya kwenda kuupumzisha katika makao yake ya milele.
Mhe. Joseph Mbilinyi (a.k.a SUGU) akiwa na baadhi ya viongozi na aliye kada wa CCM pia mfadhili wa CHADEMA ndugu; Sabodo wakielekea kutoa heshima zao za mwisho kwa marehemu Steven Charles Kanumba katika viwanja vya Leaders Club hapo jana
Mhe. Ghalib Bilali akiongoza viongozi wengine wa kiserikali na watanzania kwa ujumla katika kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa gwiji wa sanaa ya filamu Tanzania Steven Kanumba, katika viwanja vya Leaders hapo Jana.  
Baadhi ya wasanii wa filamu Tanzania wakiwa wameketi karibu kabisa na Jeneza la aliyekuwa muugizaji maarufu wa Filamu Tanzania ndg. Steven Kanumba, tayari kwa kuanza misa ya kumwombea marehemu kama wanavyoonekana pichani.
Wasanii wa Tansia ya Filamu Tanzania wakiwa wamezunguka Jeneza la mpendwa wao Steven Charles Kanumba huku wakijadili jambo, mara baada ya kuuwasilisha mwili huo katika viwanja vya Leaders Club kwa ajili ya kuutolea heshima za mwisho.
Steven Nyerere aliyebeba msalaba wa wajina wake marehemu Steven Charles Kanumba walipokuwa wakiuingiza mwili wa marehemu katika viwanja vya leaders kwa ajili ya kutoa heshima zao za mwisho.
Kwaya ambayo marehemu Steven Charles Kanumba aliyokuwa ni mshiriki ikiimba na kuomboleza katika msiba huo, ambapo marehemu alikuwa akiagwa na watanzania wote kwa ujumla.
Mwili wa marehemu Steven Charles Kanumba ukiwa tayari kwa kuombewa mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Leaders Club hapo jana.
Mwili wa aliyekuwa Gwiji wa sanaa za uigizaji wa Filamu Tanzania Steven Charles Kanumba ukiwa umebebwa na baadhi ya wasanii wenzake wa Tansia hiyo ya Filamu mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Leaders Clubu hapo jana.
Dada wa marehemu Steven Charles Kanumba akisaidiwa na baadhi ya wasanii mara baada ya kuwasili viwanja vya Leaders huku akiwa ajiwezi kutokana na majonzi makubwa ya kuondokewa na mpendwa kaka yake.
Hili ndilo Jukwaa Kuu ambalo walilokuwa wameketi waheshimiwa Viongozi waliojitokeza ili kuuaga mwili wa Marehemu Steven Charles Kanumba siku ya Jumanne katika viwanja vya Leaders Club.
Mhe. Ghalib Bilali, Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, naye akiwasiri katika viwanja vya Leaders Club kwa kumuaga Mpendwa wetu Steven Charles Kanumba. Makamu wa Rais ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika shughuli hiyo.
Mhe. M. Sadick-Mkuu wa Mko wa Dar-es-Salaam, akiongozana na Mhe. Zungu Mbunge wa Ilala, akiwa anawasili katika viwanja hivyo vya leaders kwa ajili ya kumuuaga marehemu Steven Charles Kanumba.

Maelfu ya Watanzania wafurika kwenye viwanja vya Leaders Club - Kinondoni kumuaga na kumzika mpendwa wao STEVEN CHARLES KANUMBA

Mama Mzazi wa aliyekuwa msanii gwiji wa Filamu - Tanzania Ndg. Steven Charles Kanumba akiwa anawasili katika viwanja vya leaders tayari kwa kuuaga mwili wa mwanae mpenzi.