Mark Youssef Basseley alipokamatwa |
Mark Youssef
Basseley mtengeneza filamu ya ‘The
Innocence of Muslims’ inayomkashifu Mtume Muhammad SAW na iliyosababisha
maandamano makubwa duniani na kupelekea vifo vya watu kadhaa pamoja na balozi
wa Marekani nchini Libya, ameachiliwa huru alhamisi amethibitisha mwanasheria
wake.
Basseley alikuwa anatumikia kifungo cha mwaka mmoja kwa kukiuka masharti ya hukumu iliyotolewa 2010 ya kosa la udanganyifu. Alikuwa akitumikia adhabu hiyo katika kituo cha magereza huko Taxes.
Basseley aliwahi kutupwa jela miaka mitatu iliyopita kutokana na utapeli wa cheki za watu kwa kutumia majina mbalimbali feki. Alikaa jela mwaka mmoja kabla ya kutolewa kwa masharti kumalizia kifungo chake uraiani.Kujihusisha kwake kutengeneza filamu hiyo, kumevunja masharti aliyopewa hivyo akarudishwa jela kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela.
Kwa sasa atakuwa chini ya usimamizi kwa muda wa miaka minne kuangalia mwenendo wake katika jamii, kwa kutorudia makosa aliyotenda au kuiumiza jamii kwa namna yoyote ile. Hata hivyo haijaeleweka wapi ataishi na itakuwaje. Basseley amekuwa akiwindwa vikali na jamii ya kiislamu kwa ajili ya kuadabishwa kwa kile alichokitenda cha kuukashifu Uislamu na Mtume Muhammad SAW.
Basseley, ambaye ni tapeli mwenye kujipa majina mbalimbali mwenye umri wa miaka 56 aliwahi kuhukumiwa kwenda jela miezi 21 nchini Marekani kwa makosa mbalimbali ya utapeli, aliingia mafichoni pamoja na familia yake baada ya maandamano ya kuipinga filamu aliyoitengenza kuzidi kupamba moto.
Basseley alijiita jina la Sam Bacile wakati wa utengenezaji wa filamu ya "The Innocence of Muslims" ambayo trela lake lenye dakina 14 liliwekwa kwenye YouTube na video zake zikimuonyesha mtu aliyeigiza kama Mtume Muhammad, akifanya mapenzi, akibaka na akiamuru kuuliwa kwa watu.
Basseley au Nakoula Basseley Nakoula, hajaonekana hadharani tangu kuitoa filamu hiyo, polisi walimsaidia kumficha kwa kwenda nyumbani kwake kuichukua familia yake ya watu wanne, kisha kumhamisha kwenda mafichoni kusikojulikana. Polisi wa Los Angeles waliwasili majira ya alfajiri kabla jua halijachomoza na walimchukua mke wa Basseley na watoto wake watatu na kuwasindikiza kwenye maficho ya siri ambako Nakoula alikuwa amejificha.
Familia
yake ilizificha sura zao wakati wakisindikwa na polisi toka kwenye nyumba yao
iliyozungukwa na waandishi wa habari wengi waliokuwa wakikesha mbele ya nyumba
hiyo.
"Tulichokifanya sisi ni kuwachukua na kuwapeleka sehemu ambayo Basseley amejificha", alisema msemaji wa polisi.
"Tulichokifanya sisi ni kuwachukua na kuwapeleka sehemu ambayo Basseley amejificha", alisema msemaji wa polisi.
Baadae
mahakama iliamuru akamatwe kwa kosa la kuvunja masharti ya hukumu aliyopewa ya
kosa la utapeli. Katika mahojiano aliyowahi kufanya na CNN Basseley
alisema, “kamwe sikufikiria filamu yangu ingeweza kusababisha maumivu kwa
watu au kufa kwa sababu ya filamu yangu.”
Anasema
alitengeneza filamu hiyo ili kuweka wazi ukweli halisi kuhusu Mtume Muhammad
SAW katika unyanyasaji wake kwa kivuli cha ishara ya Mwenyezi Mungu.
Mark Youssef Basseley picha ya kuchorwa akiwa mahakamani |
Akiwa na msanii wake aliyeigiza filamu ya Innocence of Muslims |
No comments:
Post a Comment