Askari wa Kenya wakielekea katika maduka ya WestGate |
Wakati vitisho
vikirudiwa na dhihaka kutoka kwa al-Shabaab vilivyotokea siku chache
zilizopita, Watu wa Kenya bado wanatafuta majibu ya ni kwa namna gani
uzingiraji uliosababisha umwagaji wa damu ulivyotokea katika kituo cha biashara
ya maduka ya matajiri huko Westgate Nairobi.
Kwa
sasa, taarifa zilizo nyingi za uzingiraji zimeeleweka: Jumamosi iliyopita kundi
la watu wenye silaha la al-Shabaab walivamia kituo kikubwa cha maduka, waliwaua
kikatili wanunuzi na kurusha maguruneti kwenye mkusanyiko wa raia wasio na
hatia. Hali hiyo iliyodumu kwa siku nne, watu hao wenye silaha waliawaua watu
wapatao 67 na kushikilia idadi isiyojulikana ya mateka hadi vikosi vya usalama
vya Kenya vilipopata udhibiti wa hali hiyo Jumanne.
Lakini
baada ya tukio hilo, maswali mengi yalibakia bila majibu: Nini kilichotokea kwa
mateka waliobakia? Washambuliaji waliwezaje kuingia katika kituo cha maduka na
kushikilia kwa muda mrefu? Nani kiongozi katika shambulio hilo na wapi aliko
sasa?
Je,
vikosi vya usalama na vya upelelezi vilipata tahadhari kabla kuhusu shambulio,
na vingeweza kuliepusha?
"Shambulio
la kigaidi halikutokea pasipo mpango," alisema mchambuzi wa masuala ya
usalama Raymond Kipkorir Cheruiyot, kanali mstaafu wa vikosi vya jeshi la Kenya
na mmiliki shirika wa kampuni ya Multi Security Consultants Limited huko
Nairobi.
"Magaidi
walitekeleza shambulio wakati wakala wa usalama wakiwa kwenye
kujiridhisha," aliiambia Sabahi. "Maduka ya biashara ya matajiri ya
Westgate yalikuwa kwenye jengo lenye hadhi kubwa,ambalo lililpaswa kuwa chini
ya uchunguzi imara wa usalama kwa saa 24 na kulindwa na polisi wenye silaha.
Kwa njia hiyo, mpango wa shambulio hilo ungeweza kugundulika na
kuepushwa."
Cheruiyot
alikosoa mwitikio usioungana wa serikali ya Kenya wa kile kinachoelezwa kama
shambulio lenye utata ambalo "timu yenye ufa ya magaidi" walipanga
kwa uangalifu na kulitekeleza.
Mamlaka
zinapaswa kuweka lengo lenye thamani kubwa kama hiyo chini ya uchunguzi wa
kudumu, kupitia tena mipangilio na taratibu za usalama zilizopo, na kufuatilia
wenyeji wanaowaonea huruma pamoja na au kuunga mikono ugaidi, alisema.
"Ndiyo,
muda wamwitikio wa timu ya usalama ulikuwa mzuri, lakini utendaji wao ungeweza
kuwa mzuri zaidi, kama walivyotenda kwenye tahadhari ya upelelezi ya nje kwamba
maduka ya biashara ya matajiri ya Westgate yalikuwa rahisi kulengwa na
magaidi," Cheruiyot alisema.