To Chat with me click here

Tuesday, May 13, 2014

WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII - HOMA YA DENGUE

Tangazo hili limetolewa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa Watanzania wote!
 
Mbu asadikikaye kueneza homa ya dengue, hupendelea kuuma nyakati za mchana zaidi, pia hata usiku.

Homa ya Dengue: Unayohitaji Kujua

Dengue ni ugonjwa unaoleta homa kwa muda wa siku 2 hadi 7 na huambatana na dalili zifuatazo:

- Kuumwa kwa macho.
- Kuumwa kwa kichwa.
- Maumivu ya misuli na viungo.
- Kutokwa na damu (katika fizi au pua).
- Kukwaruzika kwa urahisi. 


Huduma ya nyumbani kwa homa ya Dengue ni:

- Pata vinywaji kwa wingi mfano maji, juisi au chai.
- Tumia dawa za maumivu kupunguza homa.
- Usitumie dawa ya "Aspirin" ama "Ibuprofen" 


Nenda hospitali haraka unapoona moja ya dalili za tahadhari. Dalili za tahadhari za kuangalia baada ya homa kuondoka:

- Maumivu makali ya tumbo.
- Kutapika mfululizo.
- Kutokwa damu.
- Ngozi kupauka na kuwa baridi.
- Kudhoofika kwa mwili, usingizi mzito.
- Kizunguzungu, kuzimia.
- Kupumua kwa shida.

No comments:

Post a Comment