To Chat with me click here
Showing posts with label Mgogoro. Show all posts
Showing posts with label Mgogoro. Show all posts

Monday, September 2, 2013

UWEZO WA KIJESHI KATI YA TANZANIA NA RWANDA!

Rais wa Rwanda, Paul Kagame
Rais wa Tanzania, Jakaya kikwete














Wakati mgogoro wa kidiplomasia ukizidi kushika kasi kati ya Tanzania na Rwanda, kutokana na maraisi wa nchi hizo mbili kushindwa kuelewana, kufuatia ushauri wa Raisi wa Tanzania, Jakaya Kikwete, kumtaka Rais wa Rwanda kukutana na waasi wan chi yake (FDLR) wanaotokana na jamii ya KIHUTU wakati utawala wa Kagame ni jamii ya WATUTIS ili wamalize tofauti zao. 

Ifuatayo ni ukubwa wa maeneo, uwezo, bajeti pamoja na wingi wa majeshi kwa nchi zote mbili, ili kupima uwezo wa kila nchi na majeshi yake, endapo mzozo huu kati ya wakuu wa nchi hizi mbili hatupata ufumbuzi wa haraka na kuleteleza nchi zao kuingia vitani. Fuatilia.  

Military Power:

Tanzania
Rwanda
Military Branches
Tanzania People's Defense Force (Jeshi la Wananchi la Tanzania, JWTZ): Army, Naval Wing (includes Coast Guard), Air Defense Command (includes Air Wing), National Service (2007)
Rwanda Defense Force (RDF): Rwanda Army (Rwanda Land Force), Rwanda Air Force (Force Aerienne Rwandaise, FAR) (2013)
Military service age and obligation:
18 years of age for voluntary military service; no conscription (2012)
18 years of age for voluntary military service; no conscription; Rwandan citizenship is required, as is a 9th grade education for enlisted recruits and an A-level certificate for officer candidates; enlistment is either as contract (5-years, renewable twice) or career; retirement (for officers and senior NCOs) after 20 years of service or at 40-60 years of age (2012)
Manpower available for military service:
Males age 16-49: 9,985,445 (2010 est.)
males age 16-49: 2,625,917
Females age 16-49: 2,608,110 (2010 est.)
Manpower fit for military service:
males age 16-49: 5,860,339
Females age 16-49: 5,882,279 (2010 est.)
males age 16-49: 1,685,066
Females age 16-49: 1,749,580 (2010 est.)
Manpower reaching militarily significant age annually:
male: 512,294
Female: 514,164 (2010 est.)
male: 110,736
Female: 110,328 (2010 est.)
Military expenditures:
0.9% of GDP (2012)
country comparison to the world: 134
1.3% of GDP (2012)
country comparison to the world: 112

Chanzo: The World Factbook

Thursday, September 13, 2012

MADIWANI MWANZA WAMTUHUMU WENJE KWA USALITI

BAADHI ya madiwani na wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamesema Mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje, ndiye msaliti na mvurugaji namba moja wa chama hicho.

Wakizungumza na vyanzo vya habari hii mjini hapa jana, madiwani hao ambao hawakutaka kutajwa majina yao gazetini, walisema Wenje amekuwa akitaka kuabudiwa ndani ya chama hicho na amekuwa akiitumia nafasi yake ya ujumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA kunyanyasa viongozi, madiwani na wanachama wanaompinga.

Walisema kitendo cha Kamati Kuu ya CHADEMA kuwafukuza madiwani wawili ni kukurupuka na tayari wameungana pamoja na kumtangaza Wenje kama janga ndani ya chama hicho na wanatarajia kuandaa mkutano mkubwa kwa ajili ya kuwaeleza ukweli wanachama wa Mkoa wa Mwanza.

Madiwani hao walisema Wenje amekuwa akiweka mtandao wa viongozi ndani ya CHADEMA kwa ajili ya kujiweka sawa kwa ajili ya kuwania nafasi ya uenyekiti wa mkoa na viongozi na wanachama wanaompinga amekuwa akiwazushia uasi na kutimuliwa ndani ya chama hicho.

Walisema mbunge huyo anadaiwa kupanga safu ya meya na naibu meya wa Nyamagana na Manispaa ya Ilemela.

Walisema kufukuzwa kwa Diwani wa Kitangili, Henry Matata na Diwani wa Igoma, Adamu Chagulani ni mwendelezo wa Wenje kuwatimua kwa kutumia ushawishi wake katika vikao vya uamuzi.

“Kuna kiongozi wa vijana, Robert Gwanchele, huyu alishikiwa bastola na Wenje mbele ya Dk. Slaa katika mkutano, lakini hakuna hatua zilizochukuliwa na suala liko polisi Kituo cha Kati Mwanza.

“Badala ya Wenje kuchukuliwa hatua, Gwanchele pamoja na wenzake, Deus Lutalagula, Kahayi Igweselo, Makelemo Shigemelo walifukuzwa kama mbwa ndani ya chama kutokana na kutofautiana na Wenje,” alisema mmoja wa madiwani hao.

Akizungumza na vyanzo vya habari hii, aliyekuwa Diwani wa Kitangili, Henry Matata, alisema anatarajia kutoa taarifa kwa vyombo vya habari.

“Mnapaswa msubiri na mkae mkao wa kula, nitatoa taarifa juu ya uamuzi nilioufikia na hatua ambazo nitazichukua na hatimaye iwe fundisho siku zijazo kwa watu ambao hawafuati demokrasia,” alisema Matata.

Kwa upande wake, aliyekuwa Diwani wa Igoma, Adamu Chagulani, alisema jana jioni anatarajia kufanya mkutano mkubwa kwa ajili ya kuwaeleza wananchi wa kata hiyo namna Chadema inavyoyumbishwa na Wenje na kundi lake kwa ajili ya maslahi binafsi.

“Hapa ninapozungumza niko Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro natoka Dar es Salaam kuelekea Mwanza na jioni nitakuwa na mkutano mkubwa wa hadhara kuanika kila kitu, pia ninatarajia kwenda mahakamani kupinga uamuzi wa Kamati Kuu, hiki chama si mali ya mtu fulani, ni mali ya wanachama,” alisema Chagulani.

Akizungumza na vyanzo vya habari hii, Wenje alisema hababaishwi na jambo lolote linaloelekezwa kwake na kikundi fulani cha watu kutokana na uamuzi uliofikiwa na Kamati Kuu.

“Najua kila kitu ambacho kinafanyika dhidi yangu, siwezi kusema zaidi kwa kuwa hivi sasa niko katika kikao hapa Dar es Salaam,” alisema Wenje.

Toa Maoni yako kwa habari hii

Wednesday, September 12, 2012

TENDWA, CHADEMA SASA JINO KWA JINO

Msajili wa vyama vya Siasa, John Tedwa
MVUTANO kati ya Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania, John Tendwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), umechukua sura mpya baada ya chama hicho kutangaza uhasama dhidi yake kikieleza kuwa hakiko tayari kufanya naye kazi hadi atakapowaomba radhi.

Wakati Chadema kikisema hayo, Msajili huyo amejibu madai hayo akisema hatakubali kuona chama hicho kikikaidi maagizo yake, likiwamo la kusitisha Operesheni Vuguvugu la Mabadiliko (M4C), vinginevyo sheria itachukua mkondo wake.

Septemba 4, mwaka huu Tendwa alitishia kukifuta Chadema baada ya matukio ya vurugu katika mikutano yake ukiwamo ule uliofanyika Iringa na kusababisha kifo cha aliyekuwa mwandishi wa habari wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Daud Mwangosi.

Baada ya kauli hiyo, chama hicho kilijibu mapigo na kumtaka msajili huyo aanze kwanza kukifuta Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Msimamo wa Chadema
Akizungumza na waandishi wa habari juu ya maazimio ya mkutano wa dharura wa Kamati Kuu (CC) ya chama hicho kujadili hali ya siasa nchini, uliofanyika Dar es Salaam juzi, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alitangaza uadui na Tendwa akisema chama hicho hakitafanya kazi na Ofisi ya Msajili mpaka Tendwa atakapoondolewa.