To Chat with me click here

Wednesday, May 13, 2015

RAIS NKURUNZINZA APINDULIWA!!




Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi, aliyepinduliwa hivi punde toka madarakani
akiwa mazungumzoni nchini Tanzania.
Meja Jenerali Godefroid Niyombareh amewaambia waandishi wa habari mjini Bujumubura, kuwa kumeundwa kamati maalum ya kuiokoa Burundi itakayotawala taifa hilo kwa kipindi cha mpwito.

Kulingana na taarifa iliyopeperushwa na redio Isanganiro, serikali ya Nkurunziza imeon'golewa madarakani.

Meja Generali Niyombareh amesema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa rais huyo kugombea kwa  awamu ya tatu.

Jenerali huyo alitimuliwa na Nkurunziza mwezi februari anasema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa.

Kwa sasa rais Nkurunziza yuko nchini Tanzania alipokuwa anatarajiwa kujumuika na viongozi wa kanda hii ya Afrika Mashriki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu.

Wednesday, January 7, 2015

KASHFA YA ESCROW YAMNG’OA CHENGE RASMI!


Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Bajeti, Andrew Chenge

WAKATI Watanzania wakisubiri hatima ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, ambaye Rais Jakaya Kikwete alisema anamuweka kiporo kutokana na kashfa ya uchotwaji wa zaidi ya Sh bilioni 300 kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Andrew Chenge, ametangaza rasmi kuachia nafasi hiyo.
Bunge lililopita baada ya kujadili ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kuhusu miamala iliyofanyika kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa imefunguliwa Benki Kuu ya Tanzania, lilipitisha maazimio manane ikiwa ni pamoja na kuazimia kuwajibishwa viongozi wa Serikali na wale wa kamati za Bunge walioonekana kuhusika katika kashfa hiyo.
Viongozi wa kamati ambao Bunge liliazimia wawajibishwe ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Chenge, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, William Ngeleja na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Tanesco, Victor Mwambalaswa.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo tulizipata jana, Chenge alitangaza kujiuzulu nafasi yake juzi baada ya kamati yake kukutana kwenye ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam.
“Amejiuzulu jana (juzi), saa tano asubuhi wakati wa kikao cha Kamati ya Bajeti kilichokutana kwenye Ukumbi wa Mkwawa, ofisi ndogo za Bunge Dar es Salaam.
“Aliwaambia wajumbe kuwa hataki malumbano na wabunge na hataki msuguano wowote, nafasi yake kwa sasa inashikiliwa na Dk. Festus Limbu, ambaye alikuwa makamu mwenyekiti wa kamati,” alisema mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo.
Mkurugenzi wa Idara ya Shughuli za Bunge, John Joel, alipotakiwa kuthibitisha suala hilo, alisema hayuko ofisini, hivyo hawezi kuwa na jibu la moja kwa moja juu ya suala hilo.
Alisema kama Chenge mwenyewe amefikia uamuzi huo, atakuwa amempunguzia kazi Spika.
Joel alisema kujiuzulu kwake kutakuwa ni kutimiza maazimio ya Bunge jambo ambalo ni lazima litekelezwe.
Akifafanua juu ya kumpata mwenyekiti mpya wa kamati hiyo, Joel alisema mara baada ya wajumbe hao kukutana kama viongozi hawapo, jambo la kwanza ni kufanya uchaguzi.
Alisema Chenge alichaguliwa na Spika kuongoza kamati hiyo kwa kuwa ilikuwa ni kamati mpya na ambayo ni nyeti sana.
“Wajumbe wake ukiangalia wengi walitoka kwenye Kamati ya Kushauri Vyanzo Vipya vya Mapato, Spika aliomba kumchagua mtu ili apate mtu makini anayejua vyanzo vya mapato,” alisema.
Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, alipoulizwa kama ofisi yake ina taarifa za kujiuzulu kwa Chenge, alisema yupo jimboni na hana taarifa hizo ila anachojua suala la kuwajibika kwa wenyeviti waliotajwa kwenye ripoti ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) juu ya kashfa ya Escrow ni la lazima na halihitaji mtu kuandika barua ya kujiuzulu.
“Hakuna kuandika barua ya kujiuzulu, yale ni maamuzi ya Bunge, kinachotakiwa ni kamati kukaa na kuchagua viongozi wengine,” alisema.
Ndugai akizungumza alisema kamati ambazo viongozi wake walihusishwa na kashfa ya Tegeta Escrow, zitakapokutana jukumu la kwanza litakuwa ni kuchagua viongozi wapya kwani tayari chombo hicho kilishaazimia kuwawajibisha.
Katika kashfa ya Escrow, Chenge anadaiwa kupokea Sh bilioni 1.6, kutoka kwa James Rugamalira ambaye ni mmiliki wa Kampuni ya VIP Engineering iliyokuwa na asilimia 30 kwenye Kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), inayodaiwa kuuzwa kinyemela kwa Kampuni ya Pan African Power (PAP).

GARI LINALOWEZA KUJIEGESHA KWA KUTUMIA SAA!



Dereva anaporejea kutoka alikokwenda, analiamrisha gari kutoka sehemu ilikojiegesha na kuja kumchukua dereva
Hakuna kitu kibaya kama kusahau ulikoegesha gari lako katika jengo la kuegeshea magari lenye goraf nyingi.

Lakini hivi karibuni hautahihajika kupanda gorofa kutafuta gari lako kwani kampuni ya kutengeza magari ya BMW, imetangaza kuzindia kifuaa ambacho kinaweza kuyawezesha magari ya kampuni hio kujiegesha yenyewe kwa kubonyeza tu kifaa hicho.

Hata hivyo dereva wa gari hilo atalazimika kuvaa saa ya Smartphone mkononi ambayo ataibonyeza na kuiamrisha kwa sauti gari hilo kwenda kujiegesha.

Gari hilo kwa amri ya dereva litatoka liliko baada ya dereva kushuka na kwenda lenyewe kwa kuhesabu muda utakalichukua kwenda kutafuta sehemu ya kujiegesha.

Tawi la kampuni ya BMW mjini Munich, Ujerumani limezindua teknolojia hio ambayo inawezesha gari kujiegesha lenyewe.

Gari hilo linatumia miale ya Leser iliyo kujitafutia ramani ya jengo ambalo lipo. Dereva anaweza kuliamrisha gari hilo kwenda kujiegesha kwa kutumia Smartphone.

Gari hili linaweza kujiegesha lenyewe kwa kutumia
saa ya mkononi ambayo inabonyezwa na dereva
Teknolojia hio inajulikana kama ' Remote Valet Parking Assistant,' na inafanyiwa majaribio kwenye gari la BMW i3.

Badala ya kutumia GPS, teknolojia hio inatumia miale ya Laser ambayo hutengeza ramani inayolisaidia gari hilo kutafuta sehemu ya kwenda kujiegesha.

Teknolojia hiyo inaiwezesha gari hilo kuona njia na nafasi ya kujiegeshea na pia kuona vizingiti mfano kama magari ambayo hayajaegeshwa vyema. Kwa mujibi wa waliotengeza gari hilo, linaweza kujitafutia nafasi ya kujiegesha na hata kuweza kutambua sehemu ambako kuna nafasi.
 
Teknolojia hio inatengezwa sambamba na teknolojia nyinginezo zitakazoweza kuzuia gari hilo kugongana na magari mangeine.